Home Michezo KAMPUNI YA WENTWORTH GAS LTD YAWEKEZA KATIKA JAMII

KAMPUNI YA WENTWORTH GAS LTD YAWEKEZA KATIKA JAMII

0

Meneja wa mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya Wentwoth Gas Ltd, Frank Morandi (katikati) na Afisa Michezo wa Baraza la Michezo Taifa, Charles Maguzu (Kushoto) wakimkabidhi nahodha wa timu ya Arusha Rhinos, Lewis Raphael (kulia) kombe la ushindi wa Dar Rugby Touch Tournament -2022, Jijini Dar es salaam. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd ilikuwa kati ya makampuni yaliyodhamini mashindano hiyo.

Meneja wa mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya Wentwoth Gas Ltd, Frank Morandi (Katikati) pamoja na Mkurugenzi wa shirikisho la mchezo wa rugby Tanzania (TRU), Erick Mulamula (kushoto) na Mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa rugby Tanzania (TRU) Jacob Jonas katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd ilikuwa kati ya makampuni yaliyodhamini mashindano ya Dar Touch Rugby Tournament -2022.

Meneja wa mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya Wentwoth Gas Ltd, Frank Morandi (kulia) na Mwakilishi wa klabu ya Dar Leopards, Henry Jones (kushoto) wakiwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd ilikuwa kati ya makampuni yaliyodhamini mashindano ya Dar Touch Rugby Tournament -2022.

Baadhi ya washiriki wa mashindano la Dar Touch Rugby Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Timu ya Arusha Rhinos waliibuka washindi wa Dar Touch Rugby Tournament -2022 kati ya timu zaidi ya 20 zilishiriki.  Kampuni ya Wentworth Gas Ltd ilikuwa kati ya makampuni yaliyodhamini mashindano hayo.

Baadhi ya timu zilizoshiriki katika mashindano la Dar Touch Rugby Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Timu ya Arusha Rhinos waliibuka washindi wa Dar Touch Rugby Tournament -2022 kati ya timu Zaidi ya 20 yaliyoshiriki. Kampuni ya Wentworth Gas Ltd ilikuwa kati ya makampuni yaliyo dhamini mashindano hayo.

………………………

Kama sehemu ya mpango wa kuwekeza katika jamii Kampuni ya Wentwoth Gas Ltd ilikuwa kati ya wadhamini wa mashindano ya Dar Touch Rugby Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Timu ya Arusha Rhinos waliibuka washindi wa Dar Touch Rugby Tournament -2022 kati ya timu zaidi ya 20 zilizoshiriki.