


***************
Maonyesho makubwa International Afrika Expo Festival Tübingen Germany yaliyofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 4 September 2022 katika mji wa Tübingen nchini Ujerumani , Tanzania imejikuta ikitingisha onyesho hilo ikiwakilishwa na wasanii wachoraji mbali mbali wakiwemo wasanii Chilonga Hajji na Meddy ambao michoro yao imekuwa kivutio kikubwa katika maonyesho hayo,Mwingine ni Mwanamitindo Bi.Diana Magesa kutoka Tanzania ambaye ni mbunifu wa mitindo inayotokana na bidhaa za Recycling ,mbunifu Diana Magesa ambaye ametingisha na kuvutia maelfu ya watazamaji katika maonyesho hayo kutokana na kazi zake ametajwa kuwa ni “Mbunifu Rafiki wa Mazingira” ,
bendera ya Tanzania ikipeperushwa kwa wingi kulikuwa na wauza bidhaa za sanaa kama kama vinyago na sanaa zingine za mapambo kutoka Tanzania.
Bendi maarufu ya muziki wa dansi ya barani ulaya “Ngoma Africa Band” inayopiga muziki wa dansi wa Tanzania inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja nayo kama kawaida yao walitingisha jukwaa siku ya jumamosi 3 September 2022 usiku na kuwatia kiwewe washabiki wa muziki katika maonyesho hayo.
Ngoma Africa Band ni bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyofanikiwa kuteka maelefu ya washabiki na bendi hiyo inadumu kwa takribani miaka 29 sasa na mdundo wake ambao umepewa jina “Bongo Dansi” amabao unavionjo kutoka uswahilini.
Maonyesho ya Internatonal Afrika Expo Festival yanatarajiwa kufanyika tena mwaka 2023 ambayo yanaudhuriwa na vikundi vya wajasilimali,wasanii,NGOs,kutoka nchi 54 za kiafrika, kwa wale ambao wanataka kushiriki 2023 wasiliana at [email protected]