Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali katika shamra shamra za maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)yaliofanyika katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa akitoa Damu ikiwa ni Ishara ya uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali akitoa Damu katika Hafla ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume akitoa Damu katika Hafla ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa akizungumza  na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)ambapo  Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kuchangia Damu katika Shamra shamra za Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

Misururu ya watu mbalimbali waliojitokeza kuchangia Damu katika Shamra shamra za Uzinduzi wa Maadhimisho ya mwaka Mpya wa Kiislamu (1444 Hjr)kwa Watu mbali mbali kujitokeza kuchangia Damu  katika Mnara wa kumbukumbu Kisonge Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

………………………………………

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha wa watu  katika jamii

Akizungumza  mara baada ya kuchangia damu hiyo katika Mnara wa Kumbukumbu Kisonge ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu,  amesema kuchangia damu ni muhimu kwani taifa linahitaji mkubwa hivyo ni vyema jamii ikahamasika katika zoezi hilo  

Amesema kumekuwa na upungufu wa damu katika baadhi ya vituo vya matibabu jambo ambalo linahatarisha maisha ya watu kufanya hivyo kutasaidia  kuokoa uhai wananchi.

 Mkuu huyo ameishukuru Ofisi ya Mufti kwa kuaanda kufanya jambo jema la kuimarisha afya za wagonjwa  na kuweka kumbukumbu za mwaka mpya wa kiislamu wenye kuleta manufaa kwa jamii.

Nae Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali amesema kuwa wameamua kusheherekea mwaka mpya wa kiislamu kwa kuchangia damu ili  kuisaidia jamii kwani kuna uhitaji mkubwa wa damu katika vituo vya afya.

Amefahamisha kuwa  zoezi hilo ni la kwanza ambalo  limeanzia  katika Mkoa wa Mjini Magharibi na litakuwa endelevu katika Mikoa yote ili waislamu waweze kufahamu miaka ya kiislamu na kuwataka waislamu kuwa tayari kufanya zoezi hilo ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Nao wananchi wamesema kuwa kitendo cha kuchangia damu kitasaidia wagojwa wenye mahitaji  ni vyema waislamu kuunga mkono Ofisi hiyo kwa uwamuzi wake wa kuanzisha jambo hilo.

Wameeleza kuwa kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu isiishie hapo bali iwe ni njia ya kujitathmini  kwa kuazimia kufanya mabo mema ya kwani kufanya jambo zuri ni ibada kwa waislamu na jamii kwa ujumla.

“Tusisheherekee tu kuingia mwaka mpaya wa kiislamu bali pia tuangalie nini tumefanya  tulikotoka na tunakokwenda , jambo gani jema ambalo tumefanya kwa ajili ya kesho tunatakiwa kila ukiingia mwaka tuzidishe ibada kwa wingi”,walisema wachangiaji hao.

 Hata hivyo wameishauri jamii kujitokeza kuchangia kwa ajili  ya kuwasaidia wale ambao wanahitaji kwani kufanya hivyo ni ibada.