Na Silvia Mchuruza,
Bukoba, Kagera.
Ni katika maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani ambapo kitaifa nchini yamefanyika mkoani kagera katika manispaa ya Bukobajuni 22, 2022 ambapo pia mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Ni Katibu mkuu wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukukuzi Zanzibar Nd. Amour Hamil Bakari kwa niaba ya waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukukuzi Zanzibar ikiwa kilele Cha maadhimisho haya ni juni 25 mwaka huu.
Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Nd. Amour amesema kuwa mabaharia wanafanya kazi katika mazingira hatarishi kwani kundi kubwa la vijana halina ajira, na ni kazi yenye kukabiliana na hatari au majanga mbali mbali ikiwemo kupoteza maisha hivyo kuna haja kwa wadau mbali mbali kuhakikisha kundi hilo linatizamwa upya.
Amesema kuwa mabaharia na wavuvi ni watu wanaochangia sana katika mchakato wa ukuaji wa uchumi kitaifa na kimataifa licha ya ugumu wa kazi hiyo hivyo ni kundi linalopaswa kuvaliwa njuga.
Amewasisitiza wadau na wasimamizi katika suala zima la mabaharia kuzingatia na kuweka mikakati maalum kuhakikisha kwamba vijana wanaoajiliwa wanapata ajira katika meli,mishahara mizuri, kuwa na bima ili kupatiwa fidia yanapotokea majanga.
” Niwashukuru waandaaji wa shughuli hii TASAC na serikali inatambua mchango mkubwa katika sekta ya bahari na pia inatambua changamoto zao ambapo asilimia 90 ya bidhaa ulimwenguni zinasafirishwa kwa kupitia usafiri wa majini”alisema katibu mkuu huyo.
Ameongeza kuwa mabaharia wanatakiwa kujenga ujasiri wa kueleza changamoto wanazokumbana nazo katika kazi zao kwa wadau wengine, wamiliki na serikali wana wajibu wa kusikiliza kwa umakini na kuzifanyia kazi changamoto hizo ili kuimalisha na kuboresha ustawi wa mabaharia kwa hali ya Sasa na baadae.
Akisoma risala ya mabaharia Nd. Hussein Nassor ambaye ni katibu mkuu wa chama cha mabaharia Zanzibar kwa niaba ya ZASU na TASU amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa ajira, mabaharia wanawake kukosa mazingira mazuri, kufanya kazi bila mikataba, kuwepo kima cha chini cha mshahara.
Aidha Nassor ameiomba serikali kuwasaidia mabaharia kupata ajira katika kampuni za nyumbani, kuziomba wizara na mamlaka zinazohusika kuruhusu wamiliki wa meli kutochukua wafanyakazi wasiokuwa na utaalam na ambao hawakusajiliwa katika vyama vya wafanyakazi.
Naye mkurugenzi mkuu mamlaka ya usafiri baharia Zanzibar Bi Sheikha Ahmed Mohamed amesema kuwa mabaharia wanafanya kazi ngumu na yenye hatari ambapo kila siku meli zinaungua moto, zinazama na kutekwa na waharifu, kufanya safari katika maeneo yenye vita kwa ajili ya kupeleka huduma muhimu ikiwemo madawa na chakula jambo linalosababisha mabaharia kupoteza maisha yao.
Hata hivyo maadhimisho kwa mwaka 2022 ni ya 12 na yamebeba kauli mbiu isemayo” Safari yako ya sasa na baadae tushirikishe.