Home Mchanganyiko WAZIRI NDUMBARO ATOA SIKU 30 KWA MAWAKILI NCHINI KUWA NA MIHURI YA...

WAZIRI NDUMBARO ATOA SIKU 30 KWA MAWAKILI NCHINI KUWA NA MIHURI YA KIELEKTONIKI

0
Waziri wa katiba na sheria ,Dokta Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha.
Rais wa chama hicho ,Dokta Edward Hosea akizungumza katika mkutano huo unaofanyika jijini Arusha.
………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro ametoa siku 30 kwa mawakili wote kuhakikisha wanakuwa na mihuri mipya  ya kielektoniki ili  kuondoa malalamiko ya watu wanaojifanya mawakili (vishoka )kwa kutumia mihuri ya mawakili hao.
 Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo   wakati akifungua mkutano mkuu wa  chama cha mawakili Tanzania (TLS)  unaofanyika jijini Arusha.
Amesema kuwa, ni lazima ndani ya siku 30  mawakili wote lazima wawe na mihuri ya kielektoniki na baada ya hapo hawatatambua mihuri mingine yoyote  ambayo sio wa kielektoniki.
“kwa miaka mingi kumekuwa na malalamiko ya watu kujifanya mawakili ambao wanafahamika kwa jina maarufu kama (vishoka) na kutumia  mihuri ya mawakili hivyo naamini kupitia mihuri ya kieletroniki ambayo imeandaliwa na TLS ambayo nimeizindua  leo  itamaliza changamoto hiyo.”amesema Dokta Ndumbaro.
“ndani ya siku 30 lazima mawakili wote wawe na mihuri  na tutaandikia mamlaka zote zinazotambua mihuri ya mawakili  maelekezo  ikiwemo TRA juu ya kuhakikisha mawakili wote wanakuwa na mihuri hiyo  lengo  likiwa ni  kuondoa malalamiko ya watu wanaotumia mihuri ya mawakili.”ameongeza Dokta Ndumbaro.
Kwa upande wake Raisi wa chama cha mawakili Tanzania  (TLS) Dkt.  Edward Hosea amesema kuwa mkutano huo umewakutanisha mawakili wote kutoka Tanzania ambao ni wanachama.
Amesema  kuwa,kutakuwa na mada tofauti zitakazowasilishwa na mawakili na kwamba wamekuwa wakifanya kazi zao kwa kushirikiana na serikali ili waweze kutimiza majukumu yao kama nchi.
Dokt Hosea ameongeza kuwa, wamekuwa wakifanya mkutano huo kila mwaka na wanatarajia kujadili mada ambazo zitaleta tija na ufanisi katika chama hicho.
Hata hivyo katika mkutano huo waziri Ndumbaro ameweza kizindua mihuri ya kielektoniki,na kizindua Saccos ya mawakili.
Naye Captain Ibrahimu Bendera akitoa maelezo ya mihuri hiyo  amesema kuwa mihuri hiyo mipya itasaidia kuwadhibiti vishoka wote ambao walikuwa wanatumia mihuri ya kawaida kiholela pamoja na wale ambao walikuwa wanavunja  sheria na maadili ya taaluma ya uwakili.
Amesema kuwa, ili kuthibiti uharibifu ambao sio sahihi wameona watumie mihuri hii ya kieletroniki ili kuwadhibiti vishoka hao ambapo amesema kuwa, muhuri huo ukigonga unaweza ukaonyesha taarifa zote za mgongaji ikiwemo ya kuwa ni wakili  wawapi  je ni wakili ambaye amesajiliwa na chama  na je anafanyia kazi zake wapi.
“Sisi kama  mawakili tumekubaliana na uamuzi wa wizara waliotoa wa kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kila wakili ana tumia muhuri huo. “amesema.