Home Mchanganyiko VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

0

NA FARIDA SAID. MOROGORO. 

Vijana nchini wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zikiwemo za kielimu ili kujipatia ujuzi utakao wasaidia kuajiriwa na kujiajiri ili kujikwamua kiuchumi.

Imeelezwa kufanya hivyo wataondokana na tabia za kuilaumu serikali kwa kukosekana  kwa ajira.

Hayo yamedhihirika baada ya vijana 150  kujipatia fursa ya elimu kupitia programu ya tujiajiri inayotolewa na benki ya KCB na wabia wengine. 

Meneja wa mradi wa 2jiajiri  Betty Mruve amesema hayo alipokuwa akitoa fomu  kwa wanafunzi walio patiwa fursa ya kupata elimu ya mafunzo kwa vitendo katika Chuo Cha Veta  katika Manispaa ya Morogoro  ambapo mafunzo  yatatolewa kwa kozi za Ujenzi,Ufundi Bomba , umeme na uchomeleaji.

Mafunzo hayo yataanza May 16 mwaka huu na kudumu kwa miezi Mitatu .

Meneja huyo aliwataka vijana hao kutumia vizuri fursa walizozipata badala ya kupuuza kwani elimu hiyo itawasaidia kujiajiri na kujipatia kipato kwa maendeleo yao na taifa zima. 

“ kwakushirikiana na wanafunzi hao wataweza kuwasaidia vijana  wengi  kufikia malengo yao na kujipatia kipato ili kuondokana na utegemezi wa vijana wengi waliopo hapa nchini”  Alisema Meneja huyo.

 Naye  Bwana Exuper Banzi ambaye ni Mzazi wa mwanafunzi aliyepata fursa ya kupatiwa elimu na kupitia mradi huo na VETA  alisema  program hii itasaidia wimbi la vijana wasio na ajira kupata ajira na kukuza kipato chao. 

Pia amesema program hii pia itasaidia kuondokana na wimbi la vijana kuwa wazururaji na kujiunga na makundi ya Kihalifu