Mratibu wa Tamasha la Usiku wa Wafia Dansi Bw.Bernard James akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Green International Bw.Kessa Mwambeleko akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022 Mkuu wa Masoko wa Gwambina Lounge Bw.Sasilo Khalid akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022 Mwanamusiki wa Dansi kutoka Mapacha Music Band Bw.Jose Mara akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022 Mwanamuziki wa Dansi kutoka Waluguru Band Bw.Killa Rey akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022 Bw.Digita Mukongya ambaye ni rais wa Mjengoni Classic Band akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Usiku wa Wafia Dansi itakalofanyika katika Ukumbi wa Gwambina Lounge Mei 28,2022.
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Mo Green International inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo nchini imejikita kusaidia muziki wa dansi nchini kwa kudhamini Tamasha la Wafia Dansi linalotarajia kufanyika Mei 28,2022 katika ukumbi wa Gwambina Lounge Temeke Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam Mratibu wa Tamasha hilo, Bw.Bernard James kutoka kampuni ya Cheza Kidansi Entertainment amesema lengo la tamasha hilo ni kurudisha upya muziki huo.
Amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Chama cha Muziki wa dansi Tanzania (CHAMUDATA) kuhakikisha vinapaswa kutoa kipaumbile katika bendi za muziki wa dansi ili kufika mbali.
“Muziki huu una idadi kubwa ya mashabiki hivyo wajibu kuendelezwa ili vizazi vijavyo viweze kufahamu nyimbo zenye ujumbe nzuri na maadili ya nchi yetu, ” Amesema Bw.James.
Mratibu huyo ametaja bendi hizo ambazo ni Msondo Ngoma Music Band, Bogoss Music chini ya Nyoshi el Sadaat na Mapacha Music Band ya Jose Mara ambazo zote zinatokea Dar es Salaam.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Green International ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Bw. Kessa Mwambeleko ametoa wito kwa wadau wa muziki huo kujitokeza kwa wingi kusapoti muziki wa dansi ili kurudi kama hapo awali.
Amesema nyimbo za muziki dansi zinafanya vema na kutoa ujumbe kwa jamii kutokana na tungo zilizopo katika ngoma hizo.
Pia alieleza lengo la kudhamini tamasha hilo ni kuwapa nafasi hata wakulima kujipa nafasi ya kupata burudani ya Muziki wa dansi.
Aidha, kutakuwa na bendi mbili kutoka nje ya Dar es Salaam – Waluguru Original ya Morogoro na Mjengoni Classic ya Arusha.
Nae Mwimbaji wa bendi ya Mapacha Music Band, Jose Mara amesema amejipanga vizuri kutoa burudani nzuri kwa mashabiki zake na wadau wa muziki huo.
Sanjari na siku hiyo atazindua nyimbo zake mpya ziitwazo ‘ Nitakuwa Sawa’ na ‘Hukumu ya Mapenzi’.