*************************
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alahj Majid Mwanga amewasimamisha kazi wenyeviti wa vitongoji vitatu kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madarakani.
DC Mwanga amewataja wenyeviti hao waliowaondoa madarakani ni Kondo Pilipili Kitongoji Cha Masugu Kati,John Kalonga Kitongoji Cha Masugu,Ally Liguta Kitongoji Cha Mitalulani.
Wenyeviti hao wamesimamishwa kwa makosa ya mbalimbali ikiwemo Kuuza maeneo ya hifadhi ya misitu zaidi ya hekari 70 pamoja na mashamba ya wananchi kwa wafugaji kinyume na Sheria ya ardhi
Adha katika hatua nyingine amemtaka mtendaji wa kijiji Cha Dodoma Isanga Andrew Kazimbaya kuripoti ktk ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilosa ili akapangiwe majukumu mengine kwa kushindwa kisimamia majukumu na sheria katika kijiiji hicho.
Pia amewaagiza wataalamu wa Kata ya Magomeni wakiongozwa na Mtendaji wa kata, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mifugo na Afisa Kilimo waandae taarifa ya kina juu ya migogoro iliyosababishwa na wenyeviti na kuiwasilisha ofisi ya mkuu wa wilaya ndani ya siku Saba.
Aidha amesisitiza umujimu wa ujezi wa shule ya msingi ktk vitongoji hivyo kwani watoto wanatembea umbali mrefu kufuata shule umbali mrefu.