MMOJA wa wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alipongeza mfumo huo mpy |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa
wa Tanga wametoa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini waliosajiliwa na
kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuhusu mfumo mpya ulioboreshwa wa
uwasilishaji wa Ritani ya Kodi la Ongezeko la Thamani (VAT).
Akizungumza wakati akifungua mafunzo
hayo Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar
wakati wa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na
kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Alisema mafunzo hayo yanakuwa endelevu
kwa wilaya nyengine kuhusiana mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani
za kodi la ongezeko la thamani (VAT) kwa walipa kodi pindi yanapojitokeza
mabadiliko, marekebisho ya sheria za kodi lengo ni kukuza uelewa wa wafanyabiashara
wanapotumia mifumo kuwasilisha ritanio za kodi.
Alisema mamlaka hiyo imeanzisha mfumo
wa uwasilishaji wa Ritani ulioboreshwa na ilitoa Taarifa mwezi February mwaka
huu na kwamba kuanzia ritani za mwezi Machi za VAT ambazo zinawasilishwa mwezi
Aprili walipa kodi watapaswa kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa
ritani.
Afisa huyo alisema mfumo huo utakuwa
na faida nyingi ikiwemo urahisi kwa mtumiaji ambapo mlipakodi atahitajika
kutumia akaunti moja ya uwasilishaji wa ritani tofauti na awali ilikuwa
ikimlazimu mlipakodi kutumia tofauti kulingana na aina ya ritani ya kodi.
Aidha alisema faida nyengine ni
ujazaji wa ritani umerahisishwa ambapo taarifa za manunuzu katika ritani ya VAT
zitaingizwa kwa kutumia namba ya uthibitisho (Verfication Code) tu iliyopo
katika risiti ya kieletroniki tofauti na awali ambapo itamlazimu mlipakodi
kujaza taarifa za kadhaa kama Jina la Muuzaji, Namba ya Usajili wa VAT, Namba
na tarehe risiti/ankra, Kiasi cha Manunuzi na VAT katika manunuzi husika.
“Kwa kweli mfumo huo mpya utaongeza mapato ya
serikali na lengo la serikali ni kumrahisishia mlipakodi atape huduma
iliyoboreshwa bila kufika TRA na hivyo atapata kuwasilisha ritani akiwa ofisini
au nyumbani bila kufika TRA”Alisema
Hata hivyo alisema mfumo huo
utawezesha kufanyika kwa marekebisho ya kodi pale yanapotokea kama
yalivyoanishwa katika sheria ya kodi la ongezeko la thamani sura ya 148 tofauti
na utaratibu wa sasa ambapo mlipakodi alihitajika kuandika barua ya kutoa
taarifa kwa Kamisha.
Awali akizungumza mmoja wa
wafanyabiashara hao kutoka SD Supermarket Moniraju Vasant alisema wanashukuru
kupatiwa elimu hiyo ya mabadiliko hayo na kwamba mpango huo utakuwa ni mzuri
kwa ajili ya kuboresha mapato TRA.
Alisema pia utawapunguzia usumbufu wa
kwenda TRA kupata huduma badala yake kutumia mifumo hiyo wakiwa ofisini kwao na
hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu mengine