Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa chama cha akiba na mikopo cha
‘Machinga Saccos’ (PICHA KUTOKA MAKTABA)
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa chama cha akiba na mikopo cha
‘Machinga Saccos’ mkoa wa Dar es Salaam, Februari 20, mwaka huu.
Uzinduzi wa Machinga Saccos unakuja
ikiwa ni maelekezo ya Rais Samia alipokutana na viongozi wa Machinga mkoa wa
Dar es Salaam, Januari 25, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Machinga Taifa, Joseph Mwanakijiji alisema kuwa Saccos
hiyo itakuwa ni suluhisho kwa wafanyabishara hao watakapopata majanga
mbalimbali.
Mwanakijiji alisema kuwa swala la
mitaji kwa machinga limekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza biashara
wanazozifanya hivyo kuwepo kwa chombo hicho kutasaidia kukuza mitaji yao.
“Tumekuwa tukipata tabu namna gani ya
kukopeshwa, pamoja na mikopo yenye gharama kubwa, kwa hiyo kupitia Saccos hii
sisi machinga tutakuwa tumepata suluhisho.
“Saccos imebeba kila kitu, mitaji
tutapata hapa, bima pamoja na vitu mbalimbali hivyo natoa wito kwa wamachinga
mkoa wa Dar es Salaam waweze kujiunga kwa wingi,” amesema Lusinde.
Alisema kuwa kuzinduliwa kwa SACCOS
hiyo kutakuwa na faida ya wafanyabishara hao kuanza kukopa kwa riba nafuu tofauti
ilivyo hivi sasa ambavyo wanahangaika kupata mitaji ya kukuza biashara zao.
Mwanakijiji alisema kuwa
wafanyabiashara wadogo wadogo (MACHINGA) wanaungana na wafanyabiashara hao nchi
nzima kukifanya chombo hicho kuwa imara zaidi kwa kuwasaidia mitaji machinga
wote.
alisema kuwa wanampongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kwa kuamua
kuanzisha SACCOS ya machinga nchi nzima kwa kuwa itasaidia kukuza mitaji ya
wafanyabiasha hao.
Mwanakijiji alisema kuwa amekuwa Rais wa
kwanza kuweka historia ya kukutana kundi hilo la wafanyabiashara wadogo wadogo
na kutambua mchango wao katika kukuza uchumi wan chi.
Alisema katika siku hiyo ya uzinduzi
pia watazindua kitabu kitakachoelezea historia ya Machinga ambacho wamekipa
jina la ‘Mama wa Taifa’.
“Pamoja
na kuelezea historia ya machinga pia itamuelezea Rais wetu ambaye ni Rais wa
kwanza mwanamke hapa nchini. Tunawakaribisha wamachinga wahudhurie kwa wingi
siku hiyo,” amesema Mwanakijiji.
Mwanakijiji alisema wataendelea
kuhamasishana ili na mikoa mingine iweze kuanzisha Saccos.