Home Biashara WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE BANDA LA BRELA MLIMAN CITY KUPATIWA HUDUMA

WANANCHI WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE BANDA LA BRELA MLIMAN CITY KUPATIWA HUDUMA

0

Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma.

**********************

NA EMMNUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Wananchi mbalimbali wamejitokeza katika banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika viwanja vya Mlimani City kupatiwa huduma zikiwemo kusajiliwa majina ya biashara, kutoa leseni za biashara pamoja na utoaji wa elimu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo ambalo kauli mbiu yake “KAMILIKA 2022” , Afisa Leseni wa BRELA Bw.Robert Mashika amesema kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri kutokana na idadi kubwa ya watu waliofika kwaajili ya kupatiwa huduma zitolewazo na BRELA.

“Zoezi letu linaenda vizuri sana kuna idadi kubwa ya watu wanaofika kupata huduma, tukishawasikiza tunapata kufahamu changamoto zao na kuzifanyia kazi” Amesema  Mashika.

Amesema kutokana na huduma zao kwa mara nyingi wanazifanya kwenye mitandao, wananchi wengi wamekuwa hawana uelewa mkubwa kuhusu mitandao.

“Changamoto za Usajili wa Majina ya Biashara na Makampuni tunazimaliza hapa hapa, tunamsaidia mteja kujaza taarifa zake na kumkadhi Cheti chake hapa hapa” Amesema Bw.Mashika.

Aidha amewataka wananchi wote hususani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake kuchangamkia fursa hiyo ili kupata majibu ya maswali yao na  ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili zikiwemo mifumo ya mtandao.

Kwa upande wa wananchi waliojitokeza wamesema huduma inayotolewa na BRELA katika viwanja hivyo inaridhisha kwani hakuna usumbufu unaojitokeza kama unapokwenda kwenye ofisi zingine.

“Sikufikiri kama ningeptiwa huduma kwa haraka kwenye viwanja hivi, BRELA wamenihudumia vizuri sana lakini kilicho nifurahisha ni kupata cheti hapa hapa sikutegemea” Amesema Bw.Mussa Njikite.