Home Burudani VIKUNDI KADHAA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KILIMANJARO

VIKUNDI KADHAA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KILIMANJARO

0

……………………………………………………..

Adeladius Makwega,Moshi

Vikundi zaidi ya 11 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro vinatarajiwa kuonesha sanaa za maonesho katika Tamasha la Kilimanjaro linalotajiwa kufanyika jumamosi ya Januari 22, 2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi. 

Hayo yamesemwa na Afisa Sanaa wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tito Luhandala ambaye anaratibu vikundi hivyo vitakavyoonesha kazi hizo.

Akivitaja vikundi hivyo na wilaya vinavyotokea ndugu Luhandala alisema kutoka Wilaya ya Rombo ni Kikundi cha Ngoma Iringi, Kutoka Wilaya ya Siha Kikundi cha Osilgilai.

Kutoka Wilaya ya Same ni Lukanga Sanaa Group, Kutoka Wilaya ya Mwanga ni Kundi la Wazee Nasuro, kikundi cha Lambo daima na pia Kikundi cha Furahisha. Ametaja vikundi vingine ni kikundi Teule. Kutoka Moshi ni kundi la Rosi, Kutoka Wilaya ya Hai kikundi cha utenzi, Kutoka Wilaya Same kuna kikundi cha Gonjanza

Akizungumzia namna vikundi hivyo vitakavyotumbuiza Afisa Sanaa wa Wizara hii Bi Alice Choaji amesema kuwa vikundi vyote vitatumbuiza katika maeneo mbambali kuleta  hamasa  ya tukio hilo kuanzia siku ya mapokezi ya Mgeni Rasmi hadi katika tamasha lenyewe.