CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimeanza  mchakato wa kuandikisha wanachama wapya na kuhuisha wanachama wa zamani, ili  kuelekea kufanya uchaguzi Mkuu wa kupata viongozi wapya watakaokiongoza  chama kwa miaka minne ijayo. 

Kutokana na hali hiyo TASWA imepokea maelekezo kutoka Baraza la Michezo  nchini (BMT), kuandaa rejesta ya wanachama na kuiwasilisha BMT hadi kufikia  Februari 15 mwaka huu, kwa hatua nyingine za kupanga Uchaguzi Mkuu. 

TASWA inawaomba wanachama wake wote kuhuisha uanachama wao kwa kulipia  ada kuanzia leo Januari 17, 2022 hadi Februari 15, 2022, pia inawahamasisha  waandishi wa habari za michezo ambao si wanachama wa TASWA, lakini wanataka  kuwa wanachama wajitokeze kuomba uanachama kwa muda huo uliowekwa. 

Ili kurahisisha jambo hilo la kuandaa rejesta ya wanachama liwe na ufanisi zaidi,  kutakuwa na waratibu wawili, ambao ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba ya TASWA,  Gift Macha na Mhazini Msaidizi wa TASWA, Zena Chande watakaotekeleza jukumu  hilo chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando. 

Ni matumaini yangu waandishi wengi watashiriki katika jambo hili kwa maendeleo  ya chama chetu. 

Asanteni 

Juma Pinto 

Mwenyekiti TASWA