Home Mchanganyiko RALEIGH TANZANIA SOCIETY YAPANDA MITI 2000 KATIKA MANISPAA YA UBUNGO.

RALEIGH TANZANIA SOCIETY YAPANDA MITI 2000 KATIKA MANISPAA YA UBUNGO.

0

 

Mkurugenzi wa Manispaa
ya Ubungo Beatrice Dominic akionyesha mfano wa upandaji wa mti katika eneo la
Mbezi Luis.

Mkurugenzi wa Manispaa
ya Ubungo Beatrice Dominic akizungumza kuelezea umuhimu wa upandaji wa Miti
katika Manispaa hiyo

 

Mwenyekiti Mtendaji
Raleigh Tanzania Society Kanda ya Pwani Caryn Khan (kushoto) wakati wa zoezi la
upandaji wa miti katika eneo la Mbezi Luis Ubungo jijini Dar es salaam

Vijana wa Raleigh
Tanzania Society wakiwa pamoja na  Mwenyekiti
Mtendaji wao Kanda ya Pwani Caryn Khan kwenye picha ya pamoja baada ya zoezi la
upandaji wa miti katika eneo la Mbezi Luis (picha zote na Mussa Khalid).

………………………………

NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM 

Taasisi ya Raleigh
Tanzania Society imepanda takriban Miti zaidi ya
2000 katika eneo la Mbezi luis Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam kwa lengo
la kuyatumza mazingira na kuepukana na mabadiliko ya Tabianchi.
 

Akizungumza wakati wa zoezi la ufanyaji wa usafi sambamba na
uzinduzi wa upandaji wa Miti hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice
Dominic ameipongeza Taasisi hiyo kwa upandaji wa miti kwani itasaidia kuifanya
Halmashuri kuwa katika Hali ya Usafi.
 

Mkurugenz huyo wa Ubungo ametumia fursa hiyo kuwataka wadau na
Taasisi mbalimbali kuonyesha Ushirikiano kwa Manispaa hiyo katika zoezi la
upandaji wa miti kwani itasaidia kuipendezesha lakini pia kukabiliana na
Changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi.
 

‘Katika kufanya usafi tumeendeana na zoezi la kupanda Miti
katika eneo hili lakini itaendelea kupandwa katika maeneo mengine ya
Halmashauri nichukue nafasi hii kuwashukuru Raleigh International kwa kutoa
Miti na kuipanda katika Manispaa’amesema Mkurugenz Beatrice
 

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji Raleigh Tanzania Society
Kanda ya Pwani Caryn Khan amesema katika eneo hilo wamepanza miti 2000 na zoezi
Hilo limekuwa ni muendelezo katika maeneo mbalimbali wakiwa na lengo la
kutokomeza ukataji wa miti nchini.
 

Amesema kuwa katika kutekeza adhma yao ya upandaji wa miti pia
wanawahamasisha watu kutumia njia mbadala pasipo kukata miti hovyo kwani
kufanya hivyo ni uharibifu wa mazingira.
 

“Leo tupo hapa eneo la Mbezi Luis kwa kushirikiana na
serikali tumeanza kufanya usafi lakini sana tumepanda miti na sisi kama Raleigh
kampeni hii tunaifanya katika mikoa mitano Iringa,Dodoma Morogoro,Dar es salaam
na Mwanza ni zoezi ambalo ni endelevu ambalo tunalifanya hapa nchini’amesema
Caryn
 

Aidha Katika Kuelekea Miaka 60 ya Uhuru amewataka watanzania
kuhakikisha kuwa wanapanda miti lakini pia kutumia matumizi mbadala ya nishati
ili kukabiliana na mabadiliko yoyote ya kidunia.
 

Naye Mkuu wa Idara ya Mazingira Manispaa ya Ubungo Lar Bernad
amesema upandaji wa miti hiyo itasaidia mpaka nyakati za mvua hivyo amewaomba
wadau wengine kuendelea kushirikiana ili kutengeneza mazingira ambayo
wanayatumia kila siku.