Home Mchanganyiko MAFANIKIO YA MIAKA SITINI YA UHURU KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

MAFANIKIO YA MIAKA SITINI YA UHURU KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

0

Kuhusu Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji;

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Sera ya umwagiliaji ya Taifa ya Mwaka 2010, ilitoa Mwongozo wa
kuwepo kwa mambo mahususi kwenye uendelezwaji wa sekta ya Umwagiliaji pamoja na
mambo mengine ni kuwa na chombo cha kuboresha na kusimamia sekta ya umwagiliaji
nchini.

Kilimo cha umwagiliaji kilianzia mkoani Arusha enzi za
ukoloni, na baada ya Uhuru serikali iliendeleza mikakati mbalimbali ndipo
mipango mahuhusi ilianzishwa  chini ya
wizara husika kama Wizara ya maji na kilimo. Ameeleza Bwana Daudi Kaali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji.

Akiongea Ofisini kwake Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji, Bw. Godwin Mutahangarwa,
alisema katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Umwagiiaji, ambayo ilitoa muelekeo
wa sekta ya umwagiliaji nchini, serikali ilipeleka mapendekezo bungeni ya kuwa
na sheria inayoitwa Sheria ya Taifa ya Uanzishwaji wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji. National Irrigation Act ya
mwaka 2013.

Imeelezwa kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza
kutekeleza majukumu yake mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na uendelezwaji
utekelezwaji na kutoa utaalam na kuratibu na kuthibiti shughuli zote za
umwagilaji nchini.

Tume imekuwa ikitekeleza sheria na
miongozo na kanuni pamoja na kutoa elimu ya sheria hiyo kupitia vyombo
mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya
Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali anabainisha kuwa  Tume
ina mpango wa kuanza kutoa elimu kwa wananchi ya namna bora ya kuvuna
maji ya mvua kwa ajili kilimo cha umwagiliaji na matumizi mengine.

Anaongeza kuwa kwa kusema kuwa
lengo ni kuwawezesha  wakulima watumie
teknolojia ambazo zitawezesha matumizi madogo ya maji ikilinganishwa na sasa
ambapo bado wakulima wengi wanatumia mbinu za kizamani.

MABADILIKO
YA TABIA YA NCHI.

Kuhusu mabadiliko ya tabia ya
nchi Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa kuna mikakati kabambe, imewekwa ya  kuanza kutoa elimu na kuhamasisha wananchi
namna ya kuvuna na kutunza maji wakati wa msika ili yaweze kutumika wakati wa
kiangazi kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.

 “Kuna teknolojia za kisasa ambazo
zinatuwezesha kufanya kilimo cha umwagiliaji pale tu ambapo mmea unahitaji
maji, pamoja na umwagiliaji wa kutumia matone ili maji machache yanayopatikana
yatumike kuzalisha chakula hapa nchini,”anaeleza  Kaali.

Baadhi ya Mafanikio katika sekta ya kilimo cha Umwagiliaji katika
kipindi cha miaka 60 ya Uhuru
.

Kufikia miaka ya 2000
imelezwa kuwa, Serikali imekuwa ikiendelea kuwekeza katika miundombinu
ya kilimo cha umwagiliaji na eneo
linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji kwa sasa ni zaidi ya hekta laki sita,
(600,000) na kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji, inaendelea kupanua eneo la umwagiliaji kufikia hekta 1,200,000
ifikapo mwaka 2025.

Aidha Serikali,
imeendelea kuingiza progam
mbalimbali katika sekta ya Umwagiliaji kama vile utengenezaji wa mitambo
na maboresho ya Miundombinu ya umwagiliaji, kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha
vya ndani.

Wakulima nchini walikuwa wakilima kwa kutumia njia za
asili,Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kujenga na kuboresha Miundombinu
ya kilimo hicho na wakulima wameweza kujiunga katika skimu kupitia vyama vya
umwagilia vinavyosajiliwa na Tume ya taifa ya Umwagiliaji hali ambayo inawapa
fursa ya wao kulima katika skimu hizo nchini.

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetambulisha
Ada na Tozo kwa wakulima wa kilimo cha umwagiliaji ili kuendeleza ukarabati wa
skimu za umwagiliaji na kuzipatia matunzo, na wakulima wameendelea kupata
mafunzo mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji kupitia Technolojia mbalimbali za
kisasa zinazotumia maji kidogo,ili kuruhusu maji yaende katika shughuli
nyingine za maendeleo na ujenzi wa Taifa,kutoka na mabadiliko ya tabianchi
yanayosababisha hali ya ukame na ukosefu wa mvua za uhakika.

Ili kuweza kuhimili na kukabiliana na janga hili,Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji imekuwa na mikakati ya kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji
kama vile teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kuchimba mabwawa yatakayo
tumika katika kilimo cha umwagiliaji wakati wa kipindi cha kiangazi.

Bwana Daudi Kaali, Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia ya
sensa yaani vifaa vinavyotumika katika kilimo cha umwagiliaji ambapo mkulima
atatumia maji kidogo kwa wakati sahihi, teknolojia ambayo imefanyiwa majaribio
katika skimu za kilimo cha umwagiliaji mkoani Iringa, imenufaisha wakulima.

Katika ipindi hiki cha
miaka 60 ya Uhuru, Idara ya Usanifu na Utafiti;
imeweza kuwa kwenye nafasi kubwa ya
kusanifu miradi mbalimbali kwa kutumia wataalam wake wa ndani, tofauti na huko
nyuma ambapo Tume ya taifa ya umwagiliaji ilikuwa ikitumia wakandarasi washauri
kufanya kazi hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa
Idara hiyo, Mhandisi Gregory Chigwiye,
amesema Idara kwa kutumia wataalam wake wa ndani inaanda na
kusanifu miradi kumi, na kuweza kuokoa kiasi cha fedha cha shilingi bilioni
moja za kitanzania kama ingetumia mtaalam mshauri kutoka nje.

Mhandisi Chigwiye
alisema
kuwa,
upembuzi yakinifu umekuwa na faida nyingi katika sekta ya kilimo cha
umwagiliaji kwani, kabla ya kuanzisha miradi katika sekta ya kilimo cha
umwagiliaji, upembuzi yanikinifu unasaidia kufahamu kama mradi unaoenda
kutekelezwa unatekelezeka na utakuwa na manufaa kwa jamii.

“Tafiti hizi pia zinaweza kusaidia kufahamu kama kunaweza
kuwa athari zozote katika mazingira na kuangalia namna ya kuhimili na
kukabiliana na hali hiyo.” Alisisitiza.

Mhandisi Naomi Mcharo ni kaimu Mkuu wa Kitengo cha
uthibiti Ubora kitengo kinachohusika na uangaliaji wa ubora wa miundombinu
inayojengwa pamoja na kazi zinazofanyika katika sekta ya kilimo cha
umwagiliaji.

Mhandisi Mcharo alifafanua kuwa, katika miaka 60 ya uhuru
Idara imekuwa na jukumu la kuhakiki na kuangalia ubora ya miundombinu ya kilimo
cha umwagiliaji kuanzia kwenye mipango ya pamoja ya ujenzi.

Kwa Upande wa TEHAMA
,katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuu, Serikali imefanya
mambo mengi makubwa kama vile
kuanzisha taasisi za serikali kama vile Serikali Mtandao EGa, Mamlaka ya
Mawasilino Tanzania (TCRA) hizi zote ni Juhudi za Serikali za kuhakikisha
kwamba Teknolojia ya habari na Mawasiliano (TEHAMA) inakuwa  nyenzo muhimu kwa maendeleo ya mtanzania.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imenufaika na kuwepo kwa mfumo
wa mtandao Serikalini wenye kasi, usalama na uhakika ili kuweza kufanya shughuli
za ofisi kiufanisi zaidi.

Serikali pia imefanikisha
kuwepo kwa mkongo wa Taifa,kuwepo kwa barua pepe katika Ofisi za
umwagiliaji nchi nzima kwa njia salama iliyorahisishwa.

MIRADI KATIKA SEKTA YA
KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU

Mhandisi Ntonda Kimasa
ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya ujenzi na uendelezwaji wa Miundombinu ya
Umwagiliaji
Amesema
Serikali
Kupitia Tume ya
Taifa ya umwagiliaji imewekeza katika Miradi Mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji
kama ile ya SSIDP, iliyokarabati na kujenga miradi mikubwa ya kitaifa kama
DAKAWA na Lower Moshi, miradi ya ASDP, ERPP na TANCAID awamu ya kwanza na ya
pili.

Kwa kipindi hiki cha miaka 60 ya Uhuru uzalishaji katika
sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwa upande wa mazao ya chakula hususan zao la
mpunga umeongezeka kutoa tani 2 kwa heka kwa
hadi tani 8 hivisasa.

Pamoja na mafanikio yote haya, Tume ya Taifa ya umwagiliaji
ina endelea kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwa kutumia wataalam wa ndani
ili kuboresha utaalam katika shughuli za ujenzi kama vile wa mabwawa na
miundombinu mingine.Hataivyo tume ya Taifa ya Umwagiliaji inawashirikisha
wakandarasi wenye zoefu wa kujenga miradi mikubwa ya Umwagiliaji ili
kuharakisha Maendeleo ya sekta ya Umwagiliaji.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI
KWA SASA KINACHANGIA 24% YA CHAKULA NCHINI NA MALENGO KATIKA JAMBO HILI NI
KUCHANGIA 50% IFIKAPO MWAKA 2025.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani, Ofisini kwake jijini
Dodoma mapema leo, kuhusu Mafanikio katika sekta ya kilimo cha
umwagiliaji ndani ya kipindi cha miaka sitini ya uhuru.