Home Mchanganyiko SIDO CHUKUENI HATUA ZA KISHERIA KUWAONDOA WAPANGAJI WASIOLIPA KODI KUWAPISHA WAWEKEZAJI WENGINE

SIDO CHUKUENI HATUA ZA KISHERIA KUWAONDOA WAPANGAJI WASIOLIPA KODI KUWAPISHA WAWEKEZAJI WENGINE

0

……………………………………………..

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe ameliagiza Shirika la Kuhudumia na Viwanda Vidogo (SIDO) kuchukua hatua za kisheria kuwaondoa wapangaji wasiotumia wala kulipa Kodi majengo ya SIDO ili kupisha wawekezaji wengine hususani wawekezaji wadogo wadogo kutumia fursa hizo kuanzisha Viwanda na Biashara ndogo ili kutimiza lengo la Serikali la kuwa na uchumi wa Viwanda shindani na kuchangia katika maendeleo ya taifa na wananchi kwa ujumla.

Kigahe ameyasema hayo alipokuwa akifanya ziara ya kukagua miradi inayosimamiwa na SIDO, Mitaa ya Viwanda vya SIDO na Wajasiliamali wanaowezeshwa na SIDO – Shinyanga ili kusilikiza changamoto zao na kuona jinsi Serikali inavyoweza kuzitatua wakati wa muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Geita na Mwanza kuanzia Novemba 30 hadi Disemba 5, 2021.

Aidha, Naibu Waziri pia alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuiwezesha SIDO kutoa huduma bora kwa wajasiliamali, kuboresha Miundombinu ya barabara, maji na umeme katika mitaa ya Viwanda mkoani shinyanga pamoja na kuwawezesha wajasiliamali katika nyanja mbalimnali ili kuvutia wawekezaji na kukuza Biashara yenye tija.

Naibu Waziri alitoa rai kwa wamiliki wa Viwanda vya kuchakata mafuta ya kula kwa kutumia mbengu kuanzisha kilimo cha mkataba na wakulima wa mazao yanayotoa mbegu za mafuta ili kikabiliana na changamoto ya upungufu wa maligjafi na kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa malighafi hiyo na kuviwezesha viwanda hivyo kuzalisha mafuta ya kula kwa wingi na kukidhi mahitaji ya mafuta ya kula nchini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alitembelea Mitaa ya Viwanda ya SIDO na wajasiliamali wanaonufaika na huduma za SIDO kama vile Mikopo kupitia mifuko ya NEDF na CREDIT GUARANTEE SCHEMES, Maeneo ya kufanya kazi ambapo wanalipa kodi bei nafuu kuliko maeneo mengine, Mafunzo kwa wajasirimiali wakusindika vyakula, na Kuunganishishwa na Taasisi nyingine za Serikali kama BRELA, TBS na GCLA ili kupata vibali vya kuzalisha bidhaa zao, kuzirasimisha na kupata nembo za ubora

Viwanda vilivyotembelea na Mhe. Kigahe na ujube wake katika Mkoa wa Shinyanga ni pamoja na Kiwanda cha Gilitu Enterprises ltd kinachochakata mafuta kula kutokana mbegu za alizeti na pamba, Kiwanda cha Katemi Group kinachosindika Unga wa sembe na Mchele na Kiwanda cha Kizumbi Food Trading Co kinachosindika unga wa sembe.

Akiongea na Naibu Waziri Mmiliki wa kiwanda cha Gilitu enterprises kinachosindika mafuta ya kula ya alizeti na pamba Bw. Gilitu Makula alieleza changamoto kubwa wanaokabiliana nayo ni pamoja na uhaba wa malighafi hususani alizeti na pamba ambayo inafanya uzalishaji usifikie hata robo ya uwezo wa uzalishaji uliosimikwa kutokana na upatikanaji wa malighafi hizo kwa msimu.

Aidha Bw. Makula alimueleza Naibu waziri kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Kiwanda chake kimewekeza katika mitambo ya kisasa ywnye uwezo wa kuchakata mafuata ya kula kutoka kwenye mbegu hadi kwenye mashudi ya mbegu hizo ili kupata mafuta mengi zaidi na yenye ubora ili kukidhi mahitaji ya soko kuliko ilivyo sasa kuwa Viwanda vingi vinauwezo wa kukamua mbegu peke yake.

Naye Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Bedavenerabilisy Chamatata akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya sekta ya Viwanda na Biashara katika mkoa huo kwa Naibu Waziri alisema hadi sasa Mkoa wa Shinyanga una Viwanda 730 ambavyo vimeajiri wafanyakazi zaidi ya 10,150. Aidha alisema Maeneo ya ujenzi wa Vuwanda yametengwa na yanaendelea kuendelezwa ikiwemo bukonda industriw park-Kahama, Isaka SEZs , EPZ- Msalala na Shinyanga EPZ area na Tinde Industria Park – Shinyanga na maeneo mengine katika halmashauri za mkoa huo.

Naye Mkurugenzi wa SIDO Mhandisi Prof. Sylvester M. Mpanduji Prof Mpanduji akimkaribisha Mhe. Naibu waziri katika Ofisi za SIDO-Shinyanga alisema SIDO Shinyanga ni miongoni mwa vituo 6 nchini vya vifaa vya kisasa vya kuzalisha teknolojia hasa mashine za kisasa zenye uwezo wa kuzalisha mashine ndogo ndogo zenye ubora kwa wingi kwa bei nafuu na hivyo kutoa rai kwa wajasliamali kutumia huduma na mashine hizokikamilifu katika kuendeleza Viwanda na Biashara zao ndogondogo.

Akitoa Taarifa fupi ya huduma zinazotelewa na SIDO Dodoma kwa Naibu Waziri, Meneja wa SIDO Mkoa wa SHINYANGA Bw.Hopeness Eliya alisema SIDO imeendelea kutoa huduma mbali mbali huo ikiwemo huduma za kiufundi na maendeleo ya teknolojia, Uanzishaji wa miradi ya viwanda vidogo vijijini, Mafunzo, Ushauri na huduma za ugani, Masoko na Habari, na Huduma za fedha kwa wajasiliamali wadogo katika mkoa huo ili kuendeleza sekta ya Viwanda na Biashara na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.