Home Mchanganyiko TMDA WAKUTANA NA VIONGOZI WILAYA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE KUJENGA...

TMDA WAKUTANA NA VIONGOZI WILAYA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE KUJENGA UELEWA UKAGUZI WA DAWA,VIFAA TIBA NA VITENDANISHI

0

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Mafuku Kabeya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dkt. Gwamaka Mwabulambo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Mfamasia Msaidizi Manispaa ya Temeke Bw. Bernard Sabuni akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi kati TMDA na viongozi wa Wilaya ya Temeke na Watumishi wa halmashauri kwa ajili ya kujengeana uelewa wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

******************

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba hapa nchini (TMDA), imetoa elimu kwa watendaji Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke na halmashauri ili waweze kutekeleza majukumu kwa ufanisi ya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi ikiwemo kudhibiti wa matumizi ya tumbaku pamoja na bidhaa zisizosajiliwa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Mafuku Kabeya, amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani yanaimalisha ushirikiano katika utendaji wa ukaguzi wa dawa na vifaa tiba katika wilaya ya Temeke.

Bw. Kabeya amesema kuwa elimu wanayopewa na TMDA inakwenda kusaidia taifa ili wananchi wasipate madhara katika sekta ya utumiaji dawa na vifaa tiba.

“Ni jambo la muhimu kupata mafunzo kutoka TMDA na sisi tupo tayari kuyapokea kwa ajili ya wananchi wetu ili tuingie katika utekelezaji” amesema Bw. Kabeya.

Meneja wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko, amesema kuwa lengo la kuandaa kikao kazi na watendaji ni kutoa elimu ya bidhaa za dawa na vifaa tiba pamoja kuwaelimisha utekelezaji wa majukumu yao ya kimsingi.

Bw. Bitegeko amesema kuwa mujibu kifungu namba 121 cha sheria ya dawa, vifaa tiba imebainisha majukumu ya halmashauri wanayotakiwa kutekeleza ambayo ni ukaguzi wa maeneo yanayotoa huduma ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kufatilia ubora na usalama wa bidhaa.

“Halmashauri zina uwajibu wa kufatilia ubora na usalama, kama kuna tatizo wanatakiwa kuziondoa bidhaa sokoni pamoja na kutoa taarifa TMDA” amesema Bw. Bitegeko.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dkt. Gwamaka Mwabulambo, amesema kuwa wataendelea kusimamia na kuthibiti ubora wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika wilaya ya Temeke.

“TMDA wapo hapa kutupa ujuzi zaidi wa jinsi gani tunaweza kutekeleza majukumu kwa kuongeza ufanisi ili kuhakikisha wananchi wanapata dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyo safi na salama kwa matumuzi ya binadamu” amesema Dkt. Mwabulombo.

Dkt. Mwabulombo amebainisha kuwa kila baada ya robo mwaka Manispaa ya Temeke wanafanya ukaguzi na wakibaini kuna tatizo hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa kwa hatau.

Mfamasia Msaidizi Manispaa ya Temeke Bw. Bernard Sabuni, amesema kuwa changamoto iliyopo katika utekelezaji wa majukumu ya ukaguzi wamekuwa wakikutana baadhi ya watoa huduma kuwa na vyeti feki.

“Sasa hivi watu baada ya kuona kuuza dawa ni biashara, basi wengi wamekuwa wakitumia ujaja kubushi cheti feki, hivyo kuna utaratibu mtu akiomba kibali cha kufungua duka la dawa lazima awe na cheti orginal” amesema Bw. Sabuni.