Home Mchanganyiko WADAU WA ELIMU NCHINI WATAKIWA KUWEZEKA NGUVU KATIKA TAFITI.

WADAU WA ELIMU NCHINI WATAKIWA KUWEZEKA NGUVU KATIKA TAFITI.

0
Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha uhasibu Arusha,Dokta Mwamini Tulli akizungumza katika kongamano hilo katika chuo Cha uhasibu Arusha

Mkuu wa chuo Cha uhasibu Arusha ,Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza katika kongamano hilo chuoni hapo.

Baadhi ya wanafunzi katika chuo Cha uhasibu Njiro wakiwa katika kongamano hilo .
*******************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.WADAU  mbalimbali wa elimu nchini zikiwemo taasisi  za  Elimu ya juu  zimetakiwa kuwekeza nguvu na jitihada  katika kufanya  tafiti zitakazowezesha kutatua changamoto katika jamii .
Hayo yamesemwa  na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha  Uhasibu Arusha (IAA), Dokta Mwamini Tulli  kwenye kongamano la pili la uvumbuzi na ubunifu lililofanyika chuoni hapo.
Amesema kuwa,kama Taifa hatuwezi kuwa na jamii yenye maisha bora,iliyoelimika, inayopenda kujifunza zaidi,amani,utulivu na umoja,utawala na uongozi bora  na uchumi wenye kuhimili ushindani bila kuwa na  tafiti zinazotoa dira na mwelekeo wa Taifa letu kiuchumi na kijamii.
Amesema kuwa, kuwepo kwa tafiti nzuri  zilizofanywa na watalaamu zinasaidia Sana kupata suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii na kuweza kupatiwa ufumbuzi  wa haraka kwa maendeleo ya jamii na nchi yetu kwa ujumla.
Dokta Mwamini  amesema  kuwa,serikali iliona umuhimu wa kuandaa dira ya Maendeleo ya Taifa mwaka  2025, ili kuunganisha na kuelekeza fikra na rasilimali za Taifa la Tanzania, katika maeneo ya msingi yatakayoiwezesha nchi kustahimili ushindani wa kiuchumi na kujiimarisha. 
” kongamano hili lenye mada kuu “Kutumia Suluhishi za ubunifu kutatua Matatizo ya msingi”  limekuja wakati muafaka ambao zinahitajika jitihada shirikishi kati ya serikali,jamii,sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo, katika kutatua matatizo yanayoikabili jamii kiuchumi hivyo nakipongeza Sana chuo hiki kwa kuandaa kongamano hili ambalo ni suluhishi kwa changamoto mbalimbali” amesema .
Naye Mkuu wa Chuo cha IAA Prof.Eliamani Sedoyeka, amesema kongamano hilo la pili lina lengo la kuwakutanisha pamoja wavumbuzi,wabunifu ili kuonyesha kazi zao,kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo na hatimaye ubunifu wao ulete tija.
“Taasisi za Elimu ya juu zinawajibu wa kufanya tafiti zinazojikita kutatua changamoto za jamii na kuiwezesha kujikwamua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa ambao katika kongamano hili wataalamu watafanya mijadala yakinifu katika tafiti bunifu na vumbuzi mbalimbali na kuja na mapendekezo  ya namna ya kuendeleza teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake kwa lengo kuchochea uchumi,”amesema.
Ameongeza  kuwa, miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu kufikia mwaka 2030 ni pamoja na kukomesha umaskini,njaa,kazi bora na ukuaji wa uchumi,miji na jamii endelevu,kuwajibika, wakati wa kuzalisha,kutumia  bidhaa,kushughulikia mazingira, viwanda,ubunifu na miundombinu.
Mwisho