Home Mchanganyiko SHIGELLA ATAKA MJUMITA IELIMISHE VIJIJI VYOTE NCHINI UHIFADHI SHIRIKISHI WA MISITU

SHIGELLA ATAKA MJUMITA IELIMISHE VIJIJI VYOTE NCHINI UHIFADHI SHIRIKISHI WA MISITU

0

Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Morogoro, Anza-Amen Ndosa akifungua Mkutano wa 21 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Rahima Njaidi akizungumza katika Mkutano wa 21 wa Mtandao huo

Mgeni rasmi katika Mkutano wa 21 wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania MJUMITA, Anza-Amen Ndosa aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella, katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa MJUMITA

********************

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigella ameutaka Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) ambao unatoa elimu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ) katika vijiji zaidi ya 450 kuongeza juhudi na kuona uwezekano wa kufikia vijiji vyote nchini.

Shigella ametoa pongezi hizo leo wakati akifungua mkutano wa 21 wa Mjumita mjini Morogoro na kuwashirikisha wanachama mbalimbali wa Mjumita kutoka kanda mbalimbali nchini.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Msidizi wa Mkoa wa Morogoro anayesimamia mipango na uratibu, Anza-Amen Ndosa, Shigella alisema usimamizi shirikishi wa misitu kama wanavyofanya Mjumita kwa kusaidia kurasimisha misitu ya vijiji na kutoa elimu ya uhifadhi, kusaidia kuokoa misitu nchini.

Amesema misitu ya Tao la Mashariki, kwa mfano, ni muhimu kutokana na kuwa chazo cha maji ya mito mingi mkoani Morogoro na pia kuwa makazi wanyama, baadhi wakiwa hawapatikani kokote.

“Lakini kumekuwa na tatizo la ongezeko la ukataji wa misitu… Tanzania inapoteza hekta 460,000 kila mwaka kutokana na kilimo, hasa cha kuhamahama, kuchoma mkaa na kukatya magogo kwa njia ambazo si endelevu.

“Hatukatai watu kuvuna magogo na kuchoma mkaa ila wafutate taratibu na wafanye kwa njia endelevu. Misitu ikisimamiwa vyema na kutumika kwa njia enelevu ni chanzo kizuri cha mapato huki ikiendelea kutunza mifumo ikolojia ya maji na kunyonya hewa ukaa,” amesema.

Amesema athari za kutoweka kwa misitu ni kukaribisha maafa kama ya mafuriko na ukame na kusababisha mabadiliko ya tabianchi kama joto kali tunaloliona sasa na mvua nyingi kuliko kiasi ambazo alisema zitafuata baada ya joto la sasa.

Ameipongeza Mjumita kwa juhudi wanazofanya za kuhakikisha misitu ya asili inahifadhiwa huku ikitumiwa kwa njia endelevu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mjumita, Rahima Njaidi amesema shirika hilo lisilo la kiserikali limekuwa likifanya juhudi kuhakikisha misitu inalindwa huku wananchi wakinufaika nayo kwa njia endelevu.

“Wananchi wanafanya doria kwenye misitu yao, wanakumbana na changamoto mbalimbali, hawakati tamaa kwa sababu wanajua raslimali ni za kwao,” amesema Rahima.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mjumita, Rehama Njelekela amesema moja ya mafanikio ya Mjumita ni kuwezesha misitu 51 kutangazwa kwenye gazeti la serikali na kwamba imeleta pamoja wananchi 15,000 katika kusimamia misitu ya asili katika vijiji zaidi ya 450 huku vingine zaidi ya 30 vikifanya USMJ.

Amesema Mjumita imesaidi kuboresha maisha ya jamii kupitia ufugaji nyuki na vipepeo, kuzalisha mkaa endelevu, miradi ya kuweka na kukopa (vicoba) pamoja na kilimo hifadhi.

Amesema Mjumita iliyoanzishwa mwaka 2000 imepata tuzo mbili za kimataifa kutokana na kuhifadhi misitu ya asili, moja ikitolewa na nchi ya Sweden mwaka 2014 na nyingine ikitolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mwaka 2015.

Amesema baadhi ya changamoto wanazopitia ni upungufu wa raslimali fedha ili kuzifikia jamii nyingi zaidi na vijiji vingi kutokuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi, hali inayosababisha kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa msitu.

Changamoto nyingine, Makamu Mwenyekiti huyo ameitaja kuwa ni kanuni zilizoletwa na tangazo la serikali namba 417 (GN 417) la mwaka 2019