Home Mchanganyiko RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 20 WA TAASISI ZA FEDHA NCHINI ULIOANDALIWA...

RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 20 WA TAASISI ZA FEDHA NCHINI ULIOANDALIWA NA BOT JIJINI DODOMA

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba,akizungumza  wakati  wa  Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florens Luoga,akitoa taarifa wakati wa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya CRDB, ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa Mabenki Tanzania Bw.Abdulmajid Nsekela,akitoa salamu wakati wa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani)  wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa katika picha mbalimbali mara baada ya kufungua Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) leo November 25,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………

Na.Erick Mungele,Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amezitaka Taasisi za kifedha nchini  kuja na mapendekezo madhubuti ili kuboresha uchumi na kuongeza uwezo wa  kupunguza  umaskini kwa haraka ndani ya nchi .

Rais Samia ameyasema hayo leo November 25,2021 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) unaofanyika kwa siku mbili.

Rais Samia amesema Tanzania inaendelea na jitihada za kupunguza na Taasisi za kifedha za Kimataifa kuomba msamaha wa madeni au kurefushwa kwa madeni ili walipe polepole ama kusamehewa madeni.

Aidha amesema kuwa Tanzania  ni nchi mojawapo kati ya nchi 10 za Afrika zenye  uchumi unaokua kwa Kasi na imeweza kuwa na utulivu wa mfumuko wa bei na utulivu wa thamani ya Fedha ukilinganiaha na Fedha za nchi nyingine pia kwenye viashiria vya maendeleo ya mtu 28.6 Hadi 26.2 Kupunguza umaskini kutoaka asilimia.

“Tumeweza kuongeza uhai wa mtu kutoka umri wa kuishi wa miaka 50 hadi 66 lakini kubwa zaidi tumeweza kuingia katika uchumi wa Kati mwezi Julai 2020 na tutaendelea kuhakikisha kuwa sera zetu tunazotekeleza zinakwenda kukuza zaidi uchumi wetu ili tusirudi nyuma kutoka katika kiwango ambacho tumefikia,

“Lakini pia mipango yetu ya miaka mitano na yenyewe inaandaliwa katika mifumo ya kupeleka mbele uchumi wetu ili tuweze kuzikabili changamoto zilizopo na tuweze kuzifanyia Kazi ili zisiturudishe nyuma.”amesema Rais Samia

Hata hivyo Rais Samia  amezitaka Benki ambazo bado hazijashusha riba katika toaji wa mikopo wafanye hivyo  ili kuleta maendeleo ya haraka ya nchi 

Rais Samia ameongeza kuwa  ni vyema mkutano huo,ukajadili njia zitakazoisaidia nchi kunufaika katika technolojia na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ameyataka mabenki  kuwa wabunifu kusaidia kupata namna ya kutengeneza mipango ambayo itawasaida vijana kupata mitaji.

”Sisi kama Wizara tunawakaribisha kuleta kwetu maoni mbalimbali ili hadi tunakwenda bajeti ya pili tuwe na jambo la kisera ambalo tunaweza kulizungumzia”amesema Nchemba

Awali Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof.Florens Luoga,amesema kuwa  mkutano wa mwaka huu ni muhimu kwa sababu wadau wa sekta ya fedha wanaadhimisha miongo minne ya mkutano wa Taasisi za Fedha, tangu kuanzishwa kwake, Mei 1980.

Prof. Luoga amesema kuwa mkutano wa Taasisi za Fedha umekuwa jukwaa la wakuu wa taasisi za fedha, wasomi, na watendaji kukutana na kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya benki, sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla.

“Katika kipindi cha miongo minne iliyopita, tumeweza kufanya mikutano 19 kujadili masuala mbalimbali, ambayo kwa kiasi kikubwa yaliakisi mahitaji ya wakati huo”amesema Prof. Luoga

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya CRDB, ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa Mabenki Tanzania Bw.Abdulmajid Nsekela,amesema kuwa Sekta ya Fedha imejipanga kutumia fursa ya cope26.

”Tunaipongeza Benki kuu kuja na taarifa rasmi yakupungiza riba kwa Mabenki hivyo tunaahidi  kuwafikia watanzania wengi huku tumejikita kukuza Teknolojia  ili kuwafikia watanzania .”