Home Michezo MAN UNITED YANG’ARA UGENINI YAICHAPA 2-0 VILLARREAL NA KUTINGA 16 BORA ULAYA

MAN UNITED YANG’ARA UGENINI YAICHAPA 2-0 VILLARREAL NA KUTINGA 16 BORA ULAYA

0

TIMU ya Manchester United imeanza vyema maisha bila kocha Ole Gunnar Solskjaer baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Villarreal katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Cerámica, Villarreal.
Mabao ya Man United chini ya kocha mpya na wa muda, Michael Carrick baada ya kufukuzwa Solskjaer yamefungwa Cristiano Ronaldo dakika ya 78 na Jadon Sancho dakika ya 90 hilo likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu.
Kwa ushindi huo, United inafikisha pointi 10 na kupanda kileleni ikiizidi pointi tatu Villarreal baada ya wote kucheza mechi tano, hivyo kuingia Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.