Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba (katikati) akisaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini.Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu hafla hiyo imefanyika leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu (kushoto) wakionyesha mikataba mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Emmanuel Tutuba,akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mary Makondo,akitoa maelezo kuhusu programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

Baadhi ya watendaji wakifatilia  hafla ya utiaji wa saini ya makubaliano ya utoaji wa Fedha za mikopo ya utekelezaji wa programu ya kupanga,kupima na kumilikisha ardhi nchini hafla iliyofanyika hiyo leo November 8,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Mwigulu Nchemba amezitaka Halmashauri 55  zilizopokea mikopo ya fedha yenye thamani ya shilingi bilioni 50   kuhakikisha  wanazitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa na  kuzirudisha kwa wakati  ili Halmashauri zingine zipate fursa za kukopa. 

Akizungumza leo Novemba 8,2021,Jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini ya makubaliano wa utoaji wa fedha za mikopo ya  utekelezaji wa programu ya kupanga ,kupima na kumilikisha ardhi nchini,Waziri Nchemba amezitaka Halmashauri hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa fedha hizo.

Waziri Nchemba amesema  serikali imetoa kiasi cha sh bilioni 50 kwa halmashauri 55 nchini kupitia wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kusaidia upimaji wa ardhi kwenye maeneo yao.

Amesema  lengo la Serikali kutoa mikopo hiyo ni kuziwezesha halmashauri hizo kupima ardhi ili  kupima ardhi na kuondoa ujenzi wa holela kwenye maeneo hayo 

“Serikali itaendelea kutoa fedha hizo kutokana na hali ya bajeti itakavyokuwa imepangwa hivyo waliopata mikopo hiyo wanatakiwa kuonyesha mifano kwa wengine watakaohitaji,”amesema.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi ,William Lukuvi amesema kupitia fedha hizo Halmashauri zitaweza kutengeneza   bilioni 41 huku akitolea mfano Halmashauri ya Meru imekopa sh.bilioni 1.6 na inatarajia kuingiza sh bilioni 7.8.

Waziri Lukuvi amesema  siku za nyuma Halmashauri zilikuwa zikiomba mikopo kutoka taasisi za kifedha lakini awamu hii serikali imechuku jukumu hilo.

Amesema  mikopo hiyo imetolewa na serikali kutokana na andiko lililoandikwa na halmashauri husika kuhusu kazi za fedha hizo 

Amesema  kuwa jumla ya halmashauri 78 ziliomba mikopo hiyo lakini waliofanikiwa ni halmashauri hizo 55 na watakuwa wakitoa mikopo hiyo ku

Naye,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Ummy Mwalimu ameagiza mapato ya ndani ya maendeleo katika Halmashauri  kutumika pia katika  kupima na kupanga miji bila kutaja asilimia ambazo zinatakiwa kutengwa.

Hatua hiyo ilikuja kufuatia Waziri Lukuvi kumuomba Waziri Ummy Halmashuri zitenge fedha kidogo kwa ajili ya kupima na kupanga maeneo.

Waziri Ummy amesema kupatikana kwa fedha hizo imeongeza vipaumbele alivyokusudia kwenye utendaji wake wa kazi alivyojiwekea wakati anaingi kwenye wizara hiyo.

Amevitaja  vipaumbele hivyo kuwa ni huduma za afya ,elimu msingi ,kuwawezesha wananchi kiuchumi hasa akinamama ,walemavu na vijana,ujenzi wa miundombinu ya barabara 

Waziri Mwalimu amesema  kwa sasa ameongezewe kipaumbele cha tano kilichongezewa hiyom jana kuwa ni upimaji ardhi kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

“Upatikanaji wa fedha hizo zitaenda kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wanachi pamoja na halmashauri husika,”amesema