Afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma,Paul Makelele akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha(Happy Lazaro).
Afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki  Dodoma ,Paul Makelele akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo(Happy Lazaro)
*****************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Wadau kutoka nchi ya Tanzania na Kenya wamekutana jijini Arusha kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mikataba ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dodoma,Paul Makelele wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Makelele amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kutokana na maelekezo ya mkutano wa ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika nchini  Kenya , Nairobi Kati ya tarehe 20  hadi 24 agosti ,2021.
“katika mkutano huo ilielekezwa kwamba   Kuna mikataba ambayo haijakamilika  na haijasainiwa Kati ya Tanzania na Kenya ,hivyo ilielekezwa  kuwa   timu za pande zote mbili za wataalamu kutoka Tanzania na Kenya wakutane Tanzania  ili kuja kukamilisha majadiliano ya  mikataba hiyo na ikiwezekana isainiwe kwa miezi michache ijayo.”amesema Makelele.
Amesema kuwa, mikataba inayojadiliwa ni makubaliano kuhusu maswala ya uhamiaji,mkataba kuhusu maswala ya  kupeana wahalifu,mkataba kuhusu maswala ya kusaidiana  kwenye makosa ya jinai,mkataba kuhusu kubadilishana wafungwa kwani  kuna watanzania ambao wamefungwa nchini  Kenya na kuna wakenya ambao wamefungwa nchini Tanzania, hivyo  tukikamilisha majadiliano hayo tutaomba watanzania kuja kutumikia kifungo nchini kwetu na wakenya kuweza kutumikia kifungo nchini kwao.
Ametaja makubaliano mengine kuwa ni kuhusu maswala ya magereza na wafungwa na makubaliano kuhusu maswala ya uwekezaji.
Ameongeza kuwa, majadiliano  hayo yatadumu kwa siku tano na   yatakamilisha makubaliano na mikataba hiyo ili iweze kusainiwa  na pengine kwa miezi michache inayokuja.
Makelele amesema kuwa,mkutano  huo ni kwa ngazi ya wataalamu kutoka  uhamiaji ,magereza,wizara  ya katiba na sheria,ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali,wizara ya mambo  ya ndani ya nchi , viwanda na biashara,wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makelele ameongeza kuwa,mkutano huo pia umehudhuriwa  na Balozi waTanzania nchini Kenya John Simbachawene na Balozi wa Kenya nchini Tanzania ,  Dan Kazungu.
Amesema kuwa, baada ya mkutano huo utaimarisha zaidi  ushirikiano   wa nchi zote mbili hasa katika maeneo hayo yote muhimu .