………………………………………………………..
Na Asila Twaha, Morogoro
Timu ya mpira wa miguu ya TAMISEMI imetwaa ubingwa wa Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali SHIMIWI kwa kuichapa mabao 7-0 timu ya Wizara ya Katiba na Sheria mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro
Mchezo huo umeshuhudia na Mgeni rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku TAMISEMI wakiongoza mashambulizi kwa wapinzania hadi mapumziko TAMISEMI walikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko na mabadiliko hayo yaliwanufaisha zaidi TAMISEMI kwa kupata mabao mengine 4 mpaka kipyenga cha mwamuzi kinamalizika TAMISEMI wameibuka na ushindi wa mabao 7-0 na kutwaa taji hilo.
Katika mashindo hayo TAMISEMI Sports Club imeweza kutoa ubingwa katika michezo mbalimbali ikiwemo mchezo ya drafti ambapo mchezaji Salum Simba aliyemshinda mpinzani wake kutoka Maliasili katika mchezo wa fainali kwa alama 2 – 0.
Kwa upande wa mchezo wa riadha TAMISEMI iliibuka mshindi katika mita 100, 1500 na 800 kwa wanaume na wanawake mita 100, 400, 800 na 1500.
Mchezo wa kamba kwa wanawake TAMISEMI hawakuwa nyuma kwani walifanikiwa kushika nafasi ya tatu.
Mashindano hayo yalianza Oktoba 20, 2021 na kuzinduliwa rasmi Oktoba 23, 2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na kufungwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa Novemba 02, 2021.