Waziri wa Mifugo na Uvuvi – Mashimba Ndaki (kushoto) akishuhudia uwekaji saini ya makubaliano kati ya NMB na kampuni ya Bima ya Britam juu ya kutoa Bima kwa Wavuvi na Vyombo vyao maarufu kama Jahazi. Wanaotia Saini ni Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi(wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Raymond Komanga (tai nyekundu) katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza jana. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Bima NMB – Martin Massawe
Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi(wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Raymond Komanga(tai nyekundu) wakionesha kwa waandishi wa habari mikataba muda mfupi baada ya utiani sasa rasmi na kuzindua Bima ya Wavuvi na Vyombo vyao, katika hafla ya utiaji Saini iliyofanyika jijini Mwanza jana mbele ya waziri wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi – Mashimba Ndaki(kushoto), anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya Bima wa NMB Martin Massawe(kulia).
Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi(wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Raymond Komanga(tai nyekundu) wakibadilishana mikataba, muda mfupi baada ya utiani sasa rasmi na kuzindua Bima ya Wavuvi na Vyombo vyao, katika hafla ya utiaji Saini iliyofanyika jijini Mwanza jana mbele ya waziri wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi – Mashimba Ndaki(kushoto), anayeshuhudia ni Mkuu wa Idara ya Bima wa NMB Martin Massawe(kulia).
Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara Filbert Mponzi(wa pili kulia) akitoa maelezo ya kuhusu bima ya Jahazi kwa Waziri wa Kilimo na Uvuvi Mashimba Ndaki(wa tatu kushoto) wakati wa uzinduzi wa Bima hiyo uliofanyika jijini Mwanza Mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam Raymond Komanga(kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Yonas (wa pili kulia), na Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa NMB – Emmanuel Akonaay(kulia)
……………………………………………………………..
Na Mwandushi wetu – Mwanza
BENKI ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Britam wamezindua bima maalum ijulikanayo kama Jahazi kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Bima hiyo ilizinduliwa jana jijini Mwanza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki inalenga kutoa nafasi kwa wavuvi kupata kinga wanapopata majanga mbalimbali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, aliserma bima hiyo inawalenga wavuvi wadogo na wa kati hapa nchini.
Alisema wavuvi watakata bima ya asimilia 3 ya chombo husika cha shughuli ya uvuvi na kwamba wataweza kukingwa na majanga ya ajali, kuungua mitumbwi ama boti pamoja na watu watakaokuwa ndani ya vyombo hivyo.
Aliongeza kuwa faida nyingine za bima hiyo ni pamoja na familia ya mvuvi ama mtu aliyekuwa ndani ya chombo hicho kupewa mkono wa pole endapo kutatokea kifo pamoja na kupata ulemavu wa kudumu.
Aidha, bima hiyo itatoa gharama za matibabu kwa mvuvi pamoja na kulipwa fidia kutokana na ajali yoyote itakayompata atakapokuwa majini kwa ajili ya shughuli za uvuvi ama kando kando ya ziwa, mto, bwawa ama bahari.
Mponzi aliwataka wavuvi kufika katika ofisi za NMB kwa ajili ya kukata bima ambayo itawakinga na majanga mbalimbali wanapokuwa katika shughuli zao kwenye maziwa, mito, mabwawa na bahari.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa kampuni ya Bima ya Britam kanda ya ziwa, Said Kadabi alisema kwamba bima hiyo itawasaidia wavuvi katika kuinuka kiuchumi kwa kuwa sasa watanya kazi zao kwa kujiamini.
Alisema wanalenga kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii na kuyakatia bima ikiwamo mama lishe ili waweze kufanya shughuli zao kwa kujiamini zaidi.
Kwa upande wake, Waziri Ndaki aliwataka wavuvi kutumia fursa hiyo kukata bima ili iwasaidie kuwakinga wanapokumbwa na majanga mbalimbali.
Alisema siku za nyuma bima ilikuwa inawaangalia wavuvi wakubwa pekee na kwamba kwa sasa NMB na Britam wamekuja na aina mpya ya kuwasaidia wavuvi wadogo na wa kati.
Aliwataka wavuvi waendelee kupewa elimu ya bima ili waijue na kufanya maamuzi kwa kuwa ni njia sahihi ya kuwasaidia katika kipindi chote wanapokuwa katika shughuli zao.
Alisema NMB imedhamiria kuwainua kiuchumi wakulima, wafugaji na sasa ni zamu ya wavuvi na kwamba serikali inatambua mchango wao katika kuhakikisha makundi hayo yananufaika na mikopo inayotolewa na benki hiyo.
Alisema sekta ambazo zilikuwa zinaonekana kuwa na ‘risk’ kwa sasa zianze kufikiwa na kukatiwa bima kwa kuwa zina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi.
Waziri Ndaki alisema sekta ya uvuvi inaajiri watu milioni 4.5 na kwamba inachangia asilimia 1.7 ya pato la taifa hivyo ni kundi muhimu ambalo linatakiwa kusaidiwa ili liweze kupiga hatua.
MWISHO.