Home Siasa UVCCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTEKELEZA KWA KISHINDO ILANI YA UCHAGUZI YA...

UVCCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTEKELEZA KWA KISHINDO ILANI YA UCHAGUZI YA CCM

0

Katibu  Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichanu) leo Oktoba 26,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuwezesha kupatikana kwa fedha trilioni 1.3 kutoka IMF.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 26,2021 jijini Dodoma na Katibu  Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi,amesema kuwa wanampongeza Rais Samia  kutekeleza kwa kishindo ilani ya uchaguzi kwa kufanikisha kupatikana kwa ajira na mikopo kwa elimu ya juu na kuleta matokeo chanya kwa taifa.

“Hizi ni jitihada binafsi za Mhe. Raisi Samia kwa kufanikisha kupata hizi pesa ambazo zilitolewa kwa ajili ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uviko 19, lakini Mh Rais akaona hizi pesa azielekeza kwenye miradi ya maendeleo UVCCM tunampongeza sana” amesema Kihongosi

Aidha Kihongosi amempongeza Rais wa  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein  Ally Mwinyi kwa kusimamia Sera za Chama cha Mapinduzi na kukuza uchumi wa bluu.

“Wote tumeona anavyoendelea kutatua migogoro ya watu wa zanzibari kwa kuhakikisha wanapaa nafasi nzuri ya kufanya shughuli ambazo zinachangia uchumi wa Zanzibar kuendelea kukua” amesisitiza kihongosi.

Hivyo UVCCM inaunga mkono serikali zote mbili kwa kujitoa kikamilifu kwa kuhakikisha vijana wanainuka kiuchumi kwa kutenga asilimia 4 ya Pato laTaifa.

Katika hatua nyingine Bw.Kihongosi amekishauri  Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutoingilia kazi ya Mahakama na kuiachia ifanye  kazi yake.

Aidha ametoa raia kwa wanachama  na viongozi wa  CHADEMA kuacha kutoa kauli za uchochezi za kuishinikiza Mahakama kumuachia Mwenyekiti wao wa Taifa Freman Mbowe anayeshikiliwa kwa kesi ya ugaidi kuachiwa wanapaswa watambue nchi hii inaongozwa na misingi ya sheria na taratibu.

“Wenzetu hawa wa chama pinzani wamekuwa wakitoa kauli za kuitaka mahakama kumuachia kuongozi wa huyo hivyo tunapenda kwaambia wenzetu hawa mahakama haingiliwi waiache ifanye kazi yake ya utoaji wa haki kama kweli kiongozi huyo ameonewa au tuhuma hizo ni za kweli mahakama itatoa taarifa,”amesema Kihongosi.