Home Biashara WAKULIMA WAIPONGEZA ASA KWA MBEGU BORA.

WAKULIMA WAIPONGEZA ASA KWA MBEGU BORA.

0

Grace Davidi Mteknolojia wa Mbegu za Wakala wa Mbegu za kilimo ASA akiwa katika banda la ASA akiuza mahindi kwa mkulima wa mjini moshi 

Afisa kilimo wa Rehema Antony Wakala wa Mbegu za kilimo ASA ni miongoni m,wa waliokuwa wakiuza katika kilele cha siku ya chakula Duniani mkonia Kilimanjaro

………………………………………………………………

Na Lucas Raphael,Kilimanjaro

Wakulima wa zao la Mpunga mkoani Kilimanjaro wameipongeza Wakala wa Mbegu za kilimo ASA kwa kuendelea kuzalisha Mbegu bora za mazao mbalimbali yanayo wapa faida nyingi wakulima wa mkoa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  katika banda la maonesho ya siku ya chakula Duniani katika viwanja vya Mandela Pasua wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro  wamekuwa wakilima mazao yote baada ya kuwa na Mbegu za uhakika.

Ramadan Juma mkazi wa Moshi Mkulima wa zao la mpunga akinunua Mbegu katika zao hilo alisema Mbegu ya Mpunga aina ya SARO 5(TXD 306) ni Mbegu nzuri yenye mazao mengi huku ikilimwa kwa Kanda mbalimbali hapa Nchini. 

Alisema wakulima wote wakianza kuitumia Mbegu hiyo itawasaidia na kuongeza mavuno mengi tofauti na Mbegu wanazo tumia Mbegu za Asili.

Hamis Tambwe mkazi wa Moshi Mkulima wa mahindi alisema kuwa amekuwa akitumia Mbegu za Wakala ASA hasa Mbegu aina ya T 105 ambayo ni Mbegu mpya yenye mavuno mengi na ikistawi katika maeneo mbalimbali hapa Nchini.

“Mbegu za Wakala wa amekuwa akizilima kwa muda mrefu na kumpatia matokeo mzuri katika mavuno.”alisema

Akizungumzia Mbegu mpya ya mahindi ya T 105 inayozalishwa na Wakala wabegu ASA alisema Mbegu hiyo n mkombozi kwa wakulima wote wa Tanzania endapo wakiielewa na kuanza kuitumia.

Grace Davidi Mtekenolojia wa  Mbegu za Wakala wa Mbegu za kilimo ASA akiwa katika banda la ASA akiuza mahindi alisema Wakala anazalisha Mbegu bora zinazo thibitishwa na Taasisi za serikali iliziweze kumfikia Mkulima pasipo kuleta changamoto.

Alisema Taasisi hiyo ya serikali itaendelea kuzingatia ubora wa Mbegu zake iliziweze kuwanufaisha wakulima wote.