JAJI Mfawidhi Kanda ya Bukoba, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba inaweza ikawa inaongoza au ya pili kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji.
Jaji Mfawidhi ameyaeleza hayo mwisho mwa wiki ( Ijumaa ) mbele ya Makatibu Wakuu Watatu waliofika Mahakamani hapo katika ziara yao ya Kikazi ya kujionea shughuli za utoaji hakijinai zinavyotekelezwa katika Mahakama Kuu na Mahakama za Chini Mkaoni Kagera, mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo.
Kwa mujibu wa Jaji Mfawidhi Kilekamajenga, ongezeko la kesi za mauaji katika Mkoa huo ni suala linalofikirisha si kwa Mahakama peke yake bali pia kwa wadau wengine wanaohusika na mnyororo wa uotaji haki Jinai Mkaoni Kagera.
“Waheshimiwa Makatibu wakuu, kwanza nitoe shukrani zangu kwa ujio wenu, haijawahi kutokea kwa Mahakama yetu kutembelewa na Makatibu Wakuu Watatu kwa wakati moja. Nieleze kwamba moja ya changamoto kubwa tuliyonayo ni idadi kubwa ya kesi za mauaji” Akasema Jaji Mfawishi na kuongeza
Anaongeza kwamba, wao kama Majaji na Mahakama kwa ujumla wamekuwa wakijiuliza sababu za ongezeko la visa hivyo katika Mkoa wa Kagera, Mkoa ambao unapakana na nchi Jirani tatu, Uganda, Rwanda na Burund
“Kanda ya Bukoba inaweza kuwa ya kwanza au ya pili kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji, inafikirisha sana kwa nini kuwa na visa vingi vya mauaji”. Anaeleza Jaji Mfawidhi Kilekamajenga.
Akasema Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba hadi sasa ina kesi 249 ambazo zipo tayari kuanza kusikilizwa na kwamba, na kwamba kesi 49 kati ya hizo zitaanza kusikilizwa katika kikao maalum cha Mahakama Kuu kitakachoanza Mwezi Novemba Mwaka hu.
Akabainisha kwamba, uendeshaji wa kesi za mauaji pamoja na kwamba zipo complicated lakini zinahitaji fedha nyingi kuziendesha kulingana na idadi ya mashahidi.
Akasema , usikilizaji wa kesi kumi (10), kwa mfano unaweza kugharimu kati ya shilingi za Kitanzania milioni 20 mpaka 25 kulingana na idadi ya mashahidi hali inayopelekea kusikilizwa kwa kesi chache kutokana na ufunyu wa bajeti na hivyo kuathiri mnyororo wa uotaji haki.
na Akabainisha mbele ya Makatibu hao kwamba, usikilizaji wa kesi kumi (10) kwa mfano , zinaweza kugharimu karibu shilingi za kitanzania milioni 20 hadi 25 kutegemeana na idadi ya mashahidi.
“ Kesi za mauaji ni ngumu sana na zinahitaji fedha nyingi sana. Tuna kesi 249 za mauaji, lakini zitakazoweza kusikilizwa ni 49 tu kutonana na ufinyu wa bajeti, tunaiomba serikali ione namna ya kusaidia ili haki iweze kutendeka na kwa wakati na kupunguza msongamano usio wa lazima katika magereza yetu”. Akasisitiza Jaji Mfawidhi Imani Kilekamajenga.
Suala la kuwapo kwa matukio ya mauaji Mkoani Kagera halikuelezwa tu na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba bali pia limezungumwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Bukoba Kamishna Msaidizi Awadhi Juma Hajji.
Akizungumzia hali hiyo, RPC Awadhi Juma Hajji amesema kwa muda mfupi aliokaa Mkoani Kagera, akiwa ametokeza Zanzibar amekuwa akipokea taarifa za mauaji na kubwa linalosababisha matukio ya kuuana mkoani hapa ni wivu wa mapenzi.
Na kwa sababu hiyo ameshauri kuendelea kutolewa kwa elimu kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi lakini pia kila mwananchi katika nafasi yake anapashwa kutimiza wajibu wake ili kupunguza na kuondoa kabisa matukuo ya mauaji katika jamii.
“ Muda mfupi ambao nimekaa hapa nimekuwa nikipata taarifa za mauaji hali si nzuri sana, wajibu wetu Polisi ni kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao, ninaomba sana ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau wengine ya Hakijinai, na kila mmoja wetu akitimiza wajibu wetu, changamoto zinazoikabili jamii zitapungu.Amesisitiza RPC Hajji.
Naye Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Kagera Juma Masanja akizungumzia hali hiyo ya mauaji Mkoani Kagera, licha ya kusema visa vingine vinatisha na kushangaza kwamba mwanadamu anaweza kumfanyia hivyo mwanadamu mwenzi amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi.
“katika hili na mimi naomba nichangie, kwa kweli hali si nzuri, kesi ni nyingi, na wakati mwingine matukio mengine yanatisha na kuogofya mpaka unashangaa hivi ni mtu anaweza kufanya hivi. Niwaombe Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo mtoe elimu kwa wananchi na muwaeleze kwamba kujichukulia sheria Mkononi ni Kosa la Jinai” akasitiza Mwendesha Mashtaka Juma Masanja.
Mmomonyoka wa maadili, watu kutokuwa na hofu ya mungu, wivu wa mapenzi, ulevi wa kupindukia, na migogoro ya ardhi ambayo nayo imeelezwa kuwa ni mingi Mkoani Kagera ni baadhi ya sababu zinazoelezwa kuongeza visa ya mauaji katika mkoa huo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome, akizungumza visa hivyo, amesema takwimu za matukio hayo zinatisha na haziendani na Nchi ambao imeingia katika Uchumi wa Kati.
“Nchi yetu imeingia katika uchumi wa kati, lakini bado tunafanya mambo ambayo hayaendani na nchi iliyoingia katika uchumi wakati, tunapashwa kama jamii kubadilika na ni wazi kuna jambo linatakiwa kufanyika kwa nini jamii imeingia katika hali hii ya kuuanza” akasisitiza Profesa Mchome.
Makatibu Wakuu Sifuni Mchome ( Katiba na Sheria), John Jingu ( Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto) na Christopher Kadio ( Mambo ya Ndani) wamehitimisha ziara yao ya kikazi ya wiki moja katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Kagera.