Home Michezo AZAM FC YAJIWEKA NJIA PANDA CAF YATOA SARE NA PYRAMIDS YA...

AZAM FC YAJIWEKA NJIA PANDA CAF YATOA SARE NA PYRAMIDS YA MISRI

0

 Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Pyramids katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
Sare hiyo inawapa mzigo mzito Azam kwenye mchezo wa marudiano Oktoba 23 Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo nchini Misri timu hiyo ya kocha Mzambia, George Lwandamina ikihitaji ushindi au sare ya mabao ugenini ili kusonga mbele.