Home Mchanganyiko NMB KUWAFUNDA MACHINGA,WAJASIRIAMALI TEMEKE

NMB KUWAFUNDA MACHINGA,WAJASIRIAMALI TEMEKE

0
Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Donatus  Richard akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo
……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imesema katika kufanikisha Kampeni ya Temeke Gulio inafanikiwa watatoa mafunzo na mikopo kwa wamachinga na wajariamali wilayani humo.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard wakati akizungumza katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo na waandishi wa habari.
Richard alisema Benki ya NMB ni benki namba moja nchini hivyo imeamua kuungana na mkuu wa wilaya kutoa elimu kwa Machinga na wajasiriamali wilaya humo.
“NMB tunashirikiana na Manispaa ya Temeke katika utekelezaji wa Kampeni ya Temeke Gulio ambapo sisi tutaoa elimu na mikopo nafuu kwa wajasiriamali na wamachinga watakao kuwa tayari,” alisema.
Alisema wanaamini makundi hayo yakipata elimu sahihi kuhusu ujasiriamali na mikopo wataweza kushiriki kukopa ili kukuza biashara zao.
Meneja huyo alisema NMB inatoa mikopo ya fanikiwa inayoanzia Sh.500,000 hadi milioni 5, SME Sh.milioni 5 hadi Sh.milioni 50, mikopo ya bodaboda na bajaji.
“NMB imetenga Sh.bilioni 100 kwa ajili ya kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji nchi nzima kwa asilimia 10 tu,” alisema.
Alisema pamoja na elimu ya masuala ya fedha, wajasiliamali pia watapata fursa ya kufunguliwa akaunti zinazoendana na biashara zao kama vile fanikiwa akaunti  wekeza akaunt na akaunti za muda maalumu.
Halikadhalika Richard alisema pia wanatoa bima za magari, nyumba na vitu mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo ameipongeza benki ya NMB kwa kuamua kushirikiana na wilaya hiyo kuhakikisha kampeni ya Temeke Gulio inafanikiwa.
Mwegelo alisema anaamini kupitia mafunzo na mikopo ambayo itatolewa na NMB ni wazi Temeke itakuwa imekuza uchumi kwa watu wake.
Kwa upande mwingine DC Mwegelo alisema pamoja na NMB pia kampuni ya Cocacola na inayozalisha mafuta, mchele na tambi za Korie wameshiriki kwenye kampeni hiyo.
Kampeni  ya Temeke Gulio itashirikisha maeneo 20 ya wilaya ya Temeke ikiwemo masoko ambayo yalijengwa na Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (DMDP).