Home Mchanganyiko RORYA WAISHUKURU SERIKALI YA RAIS MAMA SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO

RORYA WAISHUKURU SERIKALI YA RAIS MAMA SAMIA KWA MIRADI YA MAENDELEO

0
……………………………………………………………….
MBUNGE wa Jimbo la Rorya Mkoani Mara, Jafari Chege Wambura amesema wanaipongeza Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo 
Jafari amesema ofisi ya Mbunge Jimbo la Rorya inapenda kuishukuru Serikali sikivu chini ya Mama yetu, Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutimiza mahitaji muhimu kwa wananchi wake ili kujikimu na kujiletea maendeleo.
Amesema kwenye sekta ya elimu ambayo ni muhimu imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.96 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 98 vipya vya madarasa ndani ya Jimbo la Rorya.
Amesema akatika sekta ya afya Jimbo la Rorya limepokea shilingi milioni 700 kwa ajili ya uboreshaji wa miradi ya Afya, ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya na uboreshaji wa mazingira ya sekta ya Afya.
“Tumepokea magari mawili, moja likiwa ni gari la wagonjwa (Ambulance) na lingine ni gari la chanjo,” amesema Jafari.
Amesema katika miundombinu, Rorya imepokea shilingi milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi ndani ya Jimbo la Rorya.
Shukrani mwa watendaji wote wa serikali kwa kuendelea kuwajibika lakini zaidi kwa wananchi wa Jimbo la Rorya kwa kuhoji wawakilishi na kufikisha kero zao ili kuongeza nguvu ya kudai maendeleo.