Home Mchanganyiko MRADI WA ALIVE AFRIKA MASHARIKI WAPANIA VIKALI KUWANUFAISHA WATOTO WA KIKE KATIKA...

MRADI WA ALIVE AFRIKA MASHARIKI WAPANIA VIKALI KUWANUFAISHA WATOTO WA KIKE KATIKA STADI ZA MAISHA

0

Mratibu wa mradi wa upimaji wa stadi za maisha Afrika la mashariki (ALIVE) Samsoni Sitta akizungumza jambo kuhusiana na mikakakati ambayo wamejiwekea katika kuwasaidia wanafunzi hususan kwa watoto wa kike.

Mwenyekiti wa bodi ya haki elimu Richard Mabala.

Dr. Joyce Kahembe kutoka TIE akitoa moja ya mada kuhisiana na mabmbo mbali mbali ambayo yatatakiwa apatiwa mtoto wa kike.

…………………………………………………………….

NA VICTOR MASANGU

KATIKA kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Kitaifa mashirika mbali mbali hapa nchini yameungana kwa pamoja kwa lengo la kuweza kusherekea siku hiyo ikiwe kwa kufanya shughuli mbali mbali za kimaendeleo sambamba na kukutana na wadau kwa lengo la kuweza  kuweka mikakati na kujadili mipango ambayo itamsaidia mtoto wa kike kukabiliana na changamoto  mbali mbali zinazomkabili.

Moja ya mipango ambayo imezungumziwa katika siku hiyo  maadhimisho ni pamoja na kuhakikisha kunatengenezwa mifumo imara ya kumwezesha mtoto wa kike kupatiwa stadi za maisha kuanzia ngazi za chini ambazo zitaweza kumsaidia kwa kiasi kikubwa katika kujitambua na kuelewa mambo mbali mbali ambayo anastahili kuyapata ikiwemo kupatiwa haki zake za msingi.

Kwa kuliona hilo Shirika lisolokuwa la kiserikali la Regional Educational Learning Initiative (RELI) kwa kushirikiana na wadau wengine mbali mbali wa maendeleo  endelevu ifikapo mwaka 2030  limekuja na mpango madhubuti kwa ajili ya kuweza kushughulikia changamoto mbali mbali zilizopo katika  sekta ya elimu kwa kuja na mfumo ambao utaweza kusaidia wanafunzi kupatiwa stadi za maisha na hatimaye kufanya kazi wenyewe kwa karne ya 21.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa upimaji wa stadi za maisha Afrika mashariki (ALIVE) Samsoni Sitta amebainisha kwamba Kongani yao kubwa waliyojiwekea katika mradi huo ni kuhakikisha wanamsaidia mtoto wa kike ili aweze kujitambua pamoja na kujifunza mambo mbali mbali anayokutana nayo katika maisha yake .

“Lengo kubwa la mradi huu ni  kuwasaidia wanafunzi wetu katika suala zima la stadi za maisha na kitu kingine kikubwa ambacho tunakiangalia ni hawa watoto wetu wa kike ambao bado wapo shuleni wanasoma waweze kufanikiwa katika maisha yao katika siku zijazo ikiwa sambamba na kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kwa hiyo mimi kama mtaratibu nitahakikisha mambo haya ya msingi yanafanikiwa,”alisema  Mratibu huyo.

Aidha katika hatua nyingine mratibu huyo aliongeza kuwa kuna mambo  makuu matatu ambayo ana imani yakisimamia na kufanyiwa utekelezaji wake kwa nguvu zote kutaweza  kumtegenezea kijana mbinu za kuweza kufika mbali zaidi kupitia elimu ya stadi za maisha kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo na viongozi wa serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya haki elimu Richard Mabala alisema kuwa  wataendelea kushirikiana kwa hali namali na wadu wengine wa maendeleo pamoja na serikali  kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kuweza kufundishwa mambo mbali mbali pindi wanapokuwa nyumbani pamoja na shuleni masuala mazima ya stadi za maisha ambayo itawasaidia kupambana na maisha.

“Jambo la msingi kwa watoto wetu wa kike kuwapatia stadi za maisha kwani naweza kusema kwamba na kutolea mfano kijiko kimoja cha sukari kwenye birika zima la Chai hauwezi kupata ladha ya chai kabisa na uchopekaji wa stadi za maisha na kwamba baadhi ya mambo Fulani Fulani hivi kama vile baioloji na uraia haiwezi kutosha kuwajengea watoto umahiri katika jambo la stadi za maisha.”alisema Mabala.

Naye mmoja wa wanafunzi anayesoma kidato cha pili katika shule ya sekondari Bundikani iliyopo Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Sifa Mapinduzi ameiomba serikali ya awamu ya sita iweke mpango wa kuona umuhimu wa stadi za maisha kuwa kama somo rasmi  linalofundishwa darasani ili kuwaongezea uelewa zaidi watoto wa kike katika suala zima la kujielewa pamoja na kujitambua.

“Serikali sasa kutokana na umuhimu wa stadi za maidha inatakiwa sasa liingizwe rasmi kama somo ambalo litakuwa linafundishwa darasani,kwa sasabu mimi baada ya kujifunza stadi za maisha kumeweza kunisaidia kwa kiwango kikubwa katika kujiamini na hata leo ndio maana naonge na nyie viongozi na watu wa kubwa nina jiamini kweli,”alisema Mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake Dr. Joyce Kahembe kutoka TIE alibainisha kwamba stadi za maisha  zimeweza kuchopekwa katika masomo ya biology pamoja na pamoja na somo la uraia lengo ikiwa ni kuwasaidi watoto wa kike kupambana na changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili katika maisha yao hivyo ni jambo ambalo linatakiwa kutiliwa mkazo zaidi.

Maadhimisho ya  siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka huu wa 2021 yamefanyika kwa mafanikio makubwa  kupitia muunganiko wa   baadhi ya mashirika  mbali mbali  yakiwemo RELI,kupitia mradi wake wa (ALIVE) pamoja na  Room to Read huku kauli mbinu yake inasema kuwa stadi za maisha ni ufunguo wa ndoto za mtoto wa kike.