Timu ya Yanga imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU kutoka Visiwani Zanzibar na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Yanga walipata bao kupitia kwa muuaji wa Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele dakika ya 41 akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Yusuph Athumani.
Mchezo huu ulikuwa mwendelezo wa maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara dhidi ya wenyeji KMC utakaopigwa uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma mnamo tarehe 19,2021.
Katika mchezo wa leo kipa Eric Johora alianza kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa katika kikosi hicho.