Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma
Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambapo umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,yalianza leo Oktobar 6,2021 hadi 9,2021 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi.Andrea Kundo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kuzindua duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambapo umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,yalianza leo Oktobar 6,2021 hadi 9,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi. Andrea Kundo amezindua duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambalo litawawezesha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kununua na kuuza bidhaa zao kwa njia ya mtandao huku akilitaka Shirika la Posta kujipanga kuteka soko la biashara Mtandaoni kwani wanamatawi 350 nchini.
Akizungumza leo,Oktoba 6,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa duka hilo ambao umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,Mhandisi Kundo amewaomba watanzania kutumia huduma za Shirika hilo kwani kwa sasa zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Mhandisi Kundo amesema Shirika hilo ndilo lenye mtandao mkubwa hivyo wanatakiwa kujipanga kwani soko la biashara mtandao lipo mikononi mwao.
“Ndani ya Nchi tuna matawi 350 hivyo kama watajipanga katika biashara ya mitandaoni soko lipo mikononi mwao tunatakiwa kuwa wabunifu kutoka na teknolojia tuliyonayo,”amesema.
Mhandisi Kundo amesema uzinduzi wa duka hilo ni matokeo ya maendeleo ya Teknolojia pia inakuja kutatua changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19.
Amesema duka hilo la posta mtandao litarahisishia wananchi waliopo maeneo ya pembezoni kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi ambapo pia italeta tija na kuongeza kipato kwa wananchi.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Zainabu Chaula ameeeleza kuwa kazi ya wizara ni kuweka miundombinu itakayoiwezesha nchi kwenda kwenye Tanzania ya kidigital na kuwaomba wananchi kutumia huduma za posta kwani ni salama.
“Nafurahi kuona tuna mafanikio umoja ni nguvu na ndio ambao utatuvusha kwani sisi tunatembea katika umoja,”amesema
Naye,Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo amesema kutokana na badiliko makubwa ya Teknolojia ambayo yanaenda kwa kasi kubwa dunia shirika la posta limekuwa likifanya mageuzi na maboresho katika utoaji wa huduma zake ili kuendana na sera za Umoja wa mashirika ya posta duniani.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,(TCRA) Dk Jabir Bakari,amesema sekta ya posta imepita katika changamoto nyingi ambapo amedai TCRA imetoa leseni 119 katika sekta ya Posta.