Home Mchanganyiko MAOFISA BRELA WATUMIA MAONESHO YA SIDO KIGOMA KUELIMISHA WAJASIRIAMALI KURASIMISHA BIASHARA, KUPATA...

MAOFISA BRELA WATUMIA MAONESHO YA SIDO KIGOMA KUELIMISHA WAJASIRIAMALI KURASIMISHA BIASHARA, KUPATA LESENI

0

Na Mwandishi Wetu,Kigoma

MAOFISA wa Wakala ya Usajili wa biashara na leseni (BRELA) wamewapatia elimu ya namna ya kurasimisha biashara na umuhimu wa usajili wa nembo za biashara na kupata Leseni kwa  wajasiliamali wadogo wanaoshiriki katika maonesho ya tatu ya SIDO Kitaifa yanayofanyika Wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Wakitoa mada kwa wajasiliamali hao, Ofisa Leseni wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Gabriel Gilangay ametoa mada kuhusu umuhimu wa kusajili jina la biashara na kampuni  kwa wajasiriamali  wanaoshiriki katika maonesho ya tatu ya SIDO kitaifa yanayofanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

Akifafanua muhimu na faida za kusajili Gilangay amesema biashara zao zitapata kulindwa kisheria, RRkutambulika na Serikali kwani  watakuwa katika kanzidata.”Pia  ukisajili biashara yako utapata mikopo ya biashara  katika mabenki, pia utapata zabuni zinazotangazwa ili kufanya biashara na kampuni na taasisi za Serikali.”

Kwa upande wake Athuman Makuka kutoka katika idara ya Miliki Bunifu (BRELA), ametoa ufafanuzi kuhusu sajili ya Alama ya Biashara na Vumbuzi ameeleza kuwa, ili uweze kupata usajili wa uvumbuzi ni lazima kitu hicho kiwe kitu kipya dunia nzima sio kwa hapa Tanzania tu.

“Na kwamba kiweze kushikika na pia uvumbuzi huo uweze kutatua changamoto katika jamii.  Uvumbuzi huo baada ya kusajiliwa na BRELA utalindwa kwa muda wa miaka ishirini na baada ya hapo itakuwa ni mali ya umma,”amesema.

Kuhusu alama za huduma na biashara kwa maana ya nembo ambayo inaweza kuwa Jina, Alama ama umbo ni lazima iwe ni ya kipekee, ili kupata usajili.”BRELA inaangalia upekee wa kitu ambacho utawasilisha kwa ajili ya kupata usajili.

“Baada ya kuwasilisha kuomba usajili wa nembo ni lazima iangaliwe kwamba isiwe inafanana na nyingine ambayo imekwisha sajiliwa hapa kwetu Tanzania.”

Faida ya usajili wa alama ya biashara na huduma ama nembo ni kwambwa unapata faida ya kulindwa kisherika, pia baada ya kusajili nembo utakaa kwa muda wa miaka saba ndipo atalipia tena.  Ada ya usajili wa nembo ni Sh. 130,000ambayo huilipi yote mara moja,

Wakati huo huo Ofisa Leseni Rajab Chambega ameelezea  upatikanaji wa aina mbili za leseni yaani leseni ya kiwanda na leseni ya biashara. Pia ametolea maelezo ya makundi mawili ya leseni ambazo zinatolewa na BRELA chini ya Wizara ya viwanda na biashara ambazo ni Leseni ya biashara kundi A na aina ya pili ni Leseni ya biashara kundi B ambazo hutolewa na Halmashauri chini ya TAMISENI

Pia ameelezea kuhusu viambata vinavyohitajika katika uombaji wa leseni kwa kutumia jina la Biashara na Makampuni pamoja na Adaza za usajili wa cheti / leseni ya kiwanda ni pamoja na  (NIDA, ama Cheti cha Kuzaliwa ama Paspot), pili uwe na Tin namba, pia uthibitisho wa eneo la biashara (mkataba wa pango) .

Maofisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA- wenye sare), wakikabidhi vyeti vya Usajili wa majina ya biashara kwa wadau waliokidhi vigezo na kupata usajili wa papo kwa papo kwenye banda la Taasisi hiyo katika maonesho ya tatu ya SIDlO Kitaifa, yanayofanyika katika uwanja wa Umoja uliopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.