Home Mchanganyiko TIMU YA WATAALAMU YAPIGA KAMBI MRADI WA MAJI WA MAKONDE, NEWALA

TIMU YA WATAALAMU YAPIGA KAMBI MRADI WA MAJI WA MAKONDE, NEWALA

0

Timu ya wataalamu wa Wizara ya Maji iliyoundwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ikiwa eneo la kazi tayari kwa kuanza kazi ya ukarabati mkubwa katika mradi wa maji wa Makonde, Newala mkoani Mtwara. Timu hiyo inajumuisha wataalamu wabobezi katika mitambo ya kusukuma maji (Pumps) na mfumo wa umeme.

Mtaalamu wa mifumo ya umeme akikagua mfumo wa umeme kubaini kiwango kinachofika katika mtambo katika mradi wa maji wa Makonde.

Mashine ya kusukuma maji namba moja katika mradi wa maji wa Makonde, Newala ikifunguliwa na wataalamu wa mitambo tayari kwa kufanyiwa ukarabati.mkubwa.

Ukaguzi wa mitambo katika mradi wa maji wa Makonde ukifanyika ambapo ipo mitambo mipya sita itafungwa ili kuongeza nguvu na kuhakikisha maji yanafwafikia wananchi kwa saa 24.