Home Mchanganyiko RC TABORA ASEMA JUMLA WAZEE 77, 064 WAMESHATAMBULIWA NA KUPATA VITAMBULISHO

RC TABORA ASEMA JUMLA WAZEE 77, 064 WAMESHATAMBULIWA NA KUPATA VITAMBULISHO

0
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akifungua Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya wazee Duniani chini ya ujumbe wa  usemao “Matumizi sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa rika zote” na kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Mkoa yaliyofanyika leo.
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Honoratha Rutanisibwa akitoa maelezo leo kuhusu madhumuni ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Kaimu Katibu Tawala Rukia Manduta akitoa maelezo ya utangulizi leo kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wazee duniani
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT) Dkt. Isack Laizer akitoa maelezo juu ya umuhimu wa chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani
Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Tabora wakiwa Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya wazee Duniani chini ya ujumbe wa  usemao “Matumizi sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa rika zote” na kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Mkoa yaliyofanyika leo

Picha na Tiganya Vincent

***********************************

NA TIGANYA VINCENT

Jumla ya Wazee 77,064 wametambuliwa na kuwapa vitambulisho vya msamaha wa malipo ya matibabu kufuatia maelekekezo ya Mwongozo wa Msamaha wa matibabu Mkoani Tabora

 

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya wazee Duniani chini ya ujumbe wa  usemao “Matumizi sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa rika zote”

Alisema kati ya hao Wazee 24,051 wamepatiwa msamaha wa kulipia gharama za matibabu yenye thamani ya shilingi milioni 161.2 kutoka katika zahanati, vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri za Mkoa wa .

 

Balozi Dkt.Batilda alisema kwa upande wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2020 hadi Juni 2021 imetoa misamaha ya matibabu bure yenye thamani ya shilingi milioni 40.9 kwa wazee 6,816.

 

Aidha Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali ya Awamu ya Sita inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali wazee kwa kuhakikisha huduma zote zinapatikana.

 

Balozi Dkt. Batilda alisema kwa kuthibitisha hilo tarehe 7 Mei 2021, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Samia Hassan Suluhu alikutana na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kwa niaba ya wazee wote na kutoa maagizo ya  kutatua changamoto zinazowakabili wazee.

 

 Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza Ofisi za wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wahakikishe wanatenga bajeti ya kutengeneza vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wasiokuwa na Bima ya Afya (NHF) au ICHF.

 

Ameongeza Ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote wahakikishe wanasimamia utoaji wa huduma bora kwenye madirisha ya wazee na kuendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa kwa wazee unakuwepo.