Home Mchanganyiko KOKA AENDELEA NA ZIARA YA JIMBO, AJIPANGA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KATA...

KOKA AENDELEA NA ZIARA YA JIMBO, AJIPANGA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KATA ZA PEMBEZONI

0
Picha za Matukio mbalimbali katika ziara ya mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka akiwa kata ya Viziwaziwa.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WANAFUNZI wanaosoma elimu ya sekondari wanapata kero ya kwenda kufuata elimu ya sekondari eneo jirani la Miembe Saba ,umbali wa km 15 kwenda na kurudi km 30 hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi kujiingiza kwenye makundi yasiyo na maadili .
Aidha wanafunzi hao hupata shida ya kutumia bodaboda sh.6,000 kwenda na kurudi na wengine wasio na uwezo kutembea kwa miguu.
Hayo yalijiri katika mkutano wa hadhara katika ziara ya mbunge ukagua wa Jimbo la mji wa Kibaha ,Silvestry Koka kwenye kata ya Viziwaziwa ambapo alianzia kukagua eneo la ujenzi wa shule ya msingi Sagale Magengeni lenye heka nne na kugharimu milioni 17 na kukagua ujenzi wa vyumba vitatu shule ya sekondari kata ya Viziwaziwa iliyogharimu zaidi ya milioni 58.
Akitoa kero hiyo diwani wa kata ya Viziwaziwa ,Mohammed Chamba alisema wanafunzi hao wanapata shida hivyo shule hiyo ya sekondari ikikamilika itakuwa mkombozi.
Chamba alieleza,pia kuna Changamoto ya ukosefu wa umeme Sagale Magengeni, tatizo la malipo ya mfumo wa kusambaziwa maji na ukosefu wa kituo Cha polisi.
“Zahanati Changamoto kubwa ya watumishi na ukosefu wa chumba Cha wakimama kujifungulia na mashamba pori yaliyokithiri”alieleza.
Nae Koka alisema ,mkakati wake ni kupigania kupeleka maendeleo na huduma za jamii katika kata za pembezoni.
Katika elimu Koka alisema ,wamejenga shule ya sekondari kwa nguvu za wananchi katika ujenzi huu alikuwa kipaombele na kuchangia milioni nne na kutoa milioni mbili kwa ajili ya choo japo kinahitaji kuboreshwa.
Alisema, Shule hii ianze haraka kabla ya lengo la kupangwa kuanza mapema mwakani .
Koka alisema shule ya msingi Sagale Magengeni kumepatikana eneo la shule ambapo bado inahitajika milioni saba ,”mbunge huyo atachangia milioni mbili ili kuanza ujenzi .
Katika afya kwenye zahanati ya Viziwaziwa mpango uliopo ni kuona maeneo ya pembezoni kunapatikana vituo vya afya ikiwemo kutanua zahanati hiyo.
Kwa upande wa wakazi wa kata ya Viziwaziwa,akiwemo Rich Shayo na Christopher Ngonyani walisema elimu ya sekondari iharakishwe ili kukomboa wanafunzi wanaosumbuka kwasasa.