Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde,akizungumza  wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyomalizika leo September 25,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde,wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyomalizika leo September 25,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia  nidhamu ya watumishi  waliochini yao ili kuhakikisha wanatenda haki  na kufuata miongozo kanuni na sheria  za utumishi wa umma
Kauli hiyo imetolewa leo September 25,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mhe. Silinde amesema amewataka kuhakikisha wanazingatia mipaka ya madaraka  na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watumishi zifuate  sheria, kanuni  na taratibu  za utendai  kazi katika utumishi wa umma na Serikali kwa ujumla.
Mhe. Silinde  amesema ni wajibu wa wakurugenzi kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ameaagiza wakurugenzi hao kutatua kero za wananchi  hasa walioko maeneo ya vijijini  ambao wengi ni masikini  kwa kuhakikisha wanapatikana kirahisi maofisini na kuondoa urasimu  usio wa lazima.
”Bado kuna maeneo fedha za Serikali zinapotea na kuingia katika mifuko ya wajanja kwa kutumia risiti za mikono, hivyo nawataka mtumie  mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato”amesema Mhe.Silinde
Aidha amewagiza kuhakikisha wanasimamia  matumizi sahihi za fedha za Serikali  na zitumike kwa  malengo yaliyokusudiwa  na kulingana  na thamani  ya fedha zilizotumika ikilinganishwa na huduma  iliyotolewa.
”Hakikisheni mnasimamia ubunifu na uhodari katika kutekeleza wajibu wenu kwa kuzingatia mipango  ya wananchi kupitia Halmashauri zenu na hakikisheni mnasimamia  utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zenu”amesema 
Hata hivyo Mhe. Silinde amesema ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi  vi vyema wakaongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za waalimu , vituo vya afya, vituo vya maji safi na salama.