Home Makala POSTA KIGANJANI,DUKA MTANDAO,HUDUMA PAMOJA KUKUZA UCHUMI

POSTA KIGANJANI,DUKA MTANDAO,HUDUMA PAMOJA KUKUZA UCHUMI

0

……………………………………………………………

Na Selemani Msuya

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) lilianzishwa mwaka 1994, ambapo hadi sasa linatoa huduma nchini kote na kujinga na mashirika mengine zaidi ya 650,000 duniani.

TPC inatoa huduma kupokea na kusambaza barua, vifurushi, kadi, magazeti, majarida, huduma ya mtandao, huduma pamoja na nyingine nyingi.

Dira ya TPC ni kuhutoa huduma ndani na nje katika ubora, kwa wakati na kueleweka.

Dhima yao shirika hili ni kutoa huduma ya bora ambayo inatambulika ulimwenguni na kukidhi malengo ya wateja.

Historia inaonesha kuwa shirika hili katika miaka ya nyuma limeweza kufanya vizuri katika utoaji huduma jambo ambalo lilichangia kufika kila eneo la nchi.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni TPC iliyumba katika kutoa huduma bora na kuwa tegemezi hali ambayo ilianza kuondoa ile dhana ya kulifanya shirika liwe chachu ya kukuza uchumi nchini.

Dunia yapo mashirika ya Posta kama MTN, Royal Mail, United States Postal Service na mengine mengi ambayo yanatajwa kuwa kichocheo kikubwa kwenye kukuza uchumi na kutoa huduma kwa jamii.

Kupitia mafanikio hayo makubwa ambayo yameonekana katika mashirika mengine duniani TPC imekuja upya ili kuhakikisha linakuwa shirika ambalo litachangia ukuaji wa uchumi nchini kwa kasi.

Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo anasema katika kufanikisha mikakati ya shirika kukukuza uchumi na kujitegemea wamekuja na huduma mpya tatu ambazo Posta Kiganjani, Vituo vya Huduma Pamoja na Duka Mtandao. 

Mbodo anasema Vituo vya Huduma Pamoja ambavyo vimezinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa vitahusisha Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Pia huduma hiyo itahusisha Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhaminia (RITA), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Halmashauri.

Mbodo anasema iwapo wizara na taasisi zote zitafungua vituo vya huduma pamoja posta ni wazi huduma nyingi wanazotoa zitapatikana kwa urahisi na kuongeza mapato yatayosaidia kukuza uchumi na kuondoa utegemezi.

Anasema kwa sasa wanafungua Vituo vya Huduma Pamoja katika mikoa 10 ambayo ni Dar es Salaam, Unguja, Chakechake, Morogoro, Tanga, Arusha, Dodoma, Mwanza, Kigoma na Mbeya.

“Hivi vituo vya huduma pamoja tumejipanga kuvitekeleza kwa awamu tatu ambapo hadi Desemba 2025 kila eneo la nchi vitapatikana,” anasema.

Anasema uanzishwaji wa huduma hizo mpya umewezesha shirika kuongeza mapato hadi kupata faida zaidi ya Sh.bilioni 3 hivyo mapinduzi hayo kwa siku zijazo yataongeza mapato zaidi.

Mbodo anasema kupitia huduma ya duka mtandao ambao inasimamiwa na shirika wamefanikiwa kupata zaidi ya Sh.milioni 300 huku Watanzania wengi wakiendelea kujisajili kutumia huduma hiyo.

Kaimu Posta Masta huyo anasema juhudi za shirika ni kuhakikisha Watanzania wengi wanajiunga na duka mtandao ili kufanya biashara zao kwa gharama ndogo ambapo TPC nayo itapata asilimia kidogo.

Mbogo anasema iwapo Watanzania watatumia shirika hilo ni wazi kuwa thamani ya TPC siku moja itakuwa kama Amazon au Ali Baba kwenye eneo hilo la duka mtanzao.

“Ukijiunga na duka mtandao asilimia 100 biashara yako ipo salama kwani ni huduma ambayo inasimamiwa na shirika letu  wenyewe,” anasema.

Kuhusu huduma ya Posta Kiganjani anasema nayo imekuwa chanjo sahihi cha mapato kwa shirika huku akiwasisitiza Watanzania kutumia huduma hizo.

Mbodo anasema Posta Kiganjani ni sanduku la barua linalotumia simu janja ambapo namba ya simu ya mteja ndio inasajiliwa kama sanduku la barua.

“Wateja binafsi watatumia nambari zao binafsi za simu kujisajili huku wateja wa makampuni na mashirika wakitumia namba za mashirika au makampuni yao kufanya usajili wa huduma za Posta Kiganjani,” anasema.

Kaimu Posta Masta anasema huduma hiyo itawezesha wateja kufuatilia barua na vifurushi vyao kujua wapi vimefika kupitia simu zao za mkononi. “Mteja anajulishwa kwa ujumbe mfupi meseji ikimtaarifu kufika kwa kifurishi chake ambapo atakuwa na haki ya kuamua apelekewe mahali alipo au afuate katika ofisi za posta zilizo karibu,” anaongeza.

Anasema endapo mteja atahitaji kupelekewa mzigo wake mahali alipo atapaswa kuchangia gharama kidogo.

Kaimu Posta Masta huyo anasema gharama za kulipitia huduma ya Posta Kiganjani kwa mtu binafsi ni Sh.14,160 na kampuni au shirika ni Sh.59,000 kwa mwaka.

Mbodo anasema pia huduma hiyo inakoa muda, inawezesha mteja kupata taarifa muda wowote, ina uhakika, inarahisisha kulipa kwa njia ya simu na mteja kupelekewa popote barua au kifurushi.

Kaimu Posta Masta Mkuu huyo anasema lengo na mikakati yao ni kuhakikisha kuwa shirika  hilo linakuwa mchangiaji mkubwa wa uchumi wa nchi kama nchi nyingine duniani zinavyofanya.

Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile anasema Serikali imetoa Sh. bilioni 7.8 kwa ajili ya kulifufua shirika hilo ambapo hadi sasa Posta wamepokea Sh. bilioni 3.9 ambazo zimeelekezwa kulifanya shirika kuwa jipya kila mahali.

“Shirika la Posta ni moja ya nguzo muhimu katika kukuza uchumi katika mukatadha huo Serikali imeamua kuwekeza Sh.bilioni 7.8 ambapo hadi sasa tumeshato Sh. bilioni 3.9 ambazo zinaendelea kufanya mapinduzi yanayoonekana sasa,” alisema Ndugulike wakati huo.

Aidha, alisema shirika hilo limepata dola milioni 150 ambapo kati ya hizo dola milioni 21 sawa na Sh.bilioni 49.5 zitatumika kuboresha Vituo vyas Huduma Pamoja hadi ifikapo mwaka 2025.

Dk.Ngugulile alisema vituo vya huduma pamoja vitasaidia kupunguza foleni ambazo zimekuwa zitokea katika maeneo mengine ya watoa huduma Serikalini.

Alisema maboresho hayo yamewezesha shirika hilo kuweza kushirikiana na mashirika ya Posta zaidi 650,000 duniani hivyo huduma kama duka mtandao na posta kidigitali zitaonekana kote duniani kwa wakati wote.

Waziri huyo alisema mafanikio ya Shirika la Posta yatawezeshwa na Watanzani wenyewe kwa kulitumia kutuma vifurushi na mizigo kupitia vyombo vyao ambavyo ni magari, bajaji na pikipiki.

Ndugulile alisema uzinduzi wa vituo hivyo vya huduma pamoja ni muendelezo Serikali kuimarisha huduma zinazotolewa na TPC.

Dk.Ngugulile alisema vituo vya huduma pamoja vitasaidia kupunguza foleni ambazo zimekuwa zitokea katika maeneo mengine ya watoa huduma Serikalini.

Waziri huyo alisema kwa kipindi cha miezi tisa shiriks hilo limefanikiwa kutoa huduma za biashara mtandao na posta kiganjani ambazo zimeanza kurejesha heshima ya shirika.

Katika kile ambacho kinaonesha Serikali imedhamiria kurejesha shirika hili kwenye ubora wake Waziri  Mkuu Majaliwa ameagiza wizara na taasisi zote za Serikali kujiunga na Vituo vya Huduma Pamoja vinavyosimamiwa na TPC.

Aidha, Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha kupitia madeni ya wadaiwa wote ili kuhakikisha wanalipa madeni yao jambo ambalo litaimarisha shirika hilo.

Majaliwa amezitaja baadhi ya taasisi ambazo zinapaswa kujiunga na vituo vya huduma pamoja kuwa ni Tume ya Ajira, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Anasema maboresho ambayo yamefanywa na shirika hilo yanapaswa kuungwa mkono na Serikali yenyewe hivyo aagiza wizara na taasisi zote zijiunge na vituo vya huduma pamoja ambavyo vinasimamiwa na shirika la serikali.

Majaliwa anasema haingii akilini wizara na taasisi zake kutumia fedha nyingi kusafirisha mizigo na vifurishi kupitia kampuni binafsi wakati TPC ipo na inatoa huduma bora.

“Natumia nafasi hii kuagiza wizara na taasisi zote za Serikali zijiunge na vituo vua huduma pamoja vya Posta ili kuweza kusafirisha mizigo na vifurushi. Haiwezekani tuendelee kutuma gari za taasisi, wizara.

Pia haikubaliki kuendelea kuyapa mashirika mengine ya posta kutoka nje kusafirisha vifurushi vyao wakati shirika letu lipo hivyo nasisitiza kuanzia sasa ambao hawajajiunga wajiunge na huduma za TPC ili tuweze kukuza uchumi,” anasema.

Anasema Shirika la Posta likitumika vizuri litachochea maendeleo ya kijamii na uchumi hivyo kufanikisha lengo la nchi kufikia uchumi wa viwanda.

Waziri Mkuu Majaliwa anasema uzinduzi huo wa Vituo vya Huduma Pamoja  ni muendelezo wa shirika kuja na huduma bora mbapo awali walizindua huduma ya Posta Kidigitali na Duka Mtandao ambazo zimeonesha matokeo chanya.

Anasema shirika hilo lilikuwa linasuasua ila kwa kinachooneka kwa sasa kinaakisi lengo la Serikali la kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati na viwanda.

“Uzinduzi wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yenye kuakisi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya      mwaka 2020 ambayo inataka shirika lifufuliwe,” anasema.

Majaliwa anasema shirika hilo lina ofisi zaidi ya 350 nchini kote hivyo ni vema taasisi za Serikali, mashirika na sekta binafsi kujiunga na posta ili kupata huduma ya pamoja kwa wakati.

Mwisho