Home Michezo MAYELE APELEKA TABU MSIMBAZI,YANGA YAIZIMA 1_0 SIMBA

MAYELE APELEKA TABU MSIMBAZI,YANGA YAIZIMA 1_0 SIMBA

0

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Timu ya Wananchi Yanga imefanikiwa kunyakuwa ubiingwa wa Ngao ya Hisani mara baada ya kuwabamiza mahasimu wao Simba Sc kwa bao 1-0 mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Benjamini mkappa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa wa haina yake hasa kwa timu zote mbiili kucheza kandanda safi japo Yanga ilikuwa inahamu sana ya kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na kukaa muda mrefu bila kulichukua kombe hilo.

Ni Fiston Mayele ambaye amepeleka kilio kwa wekundu wa Msimbazi mara baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Faridi Mussa dakika ya 11 na kuitendea haki pasi hiyo kwa kupiga mkwaju mkali ambao ulimshinda Manula na kuingia golini.

Mechi hiyo ilikuwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa ligi 2021/2022 ambao mechi kibao zitaingia dimbani wiki hii.