Home Biashara RC RUVUMA ABAINI UJANJA UJANJA UNUNUZI WA MAHINDI,AFUNGUA KITUO CHA RUHUWIKO

RC RUVUMA ABAINI UJANJA UJANJA UNUNUZI WA MAHINDI,AFUNGUA KITUO CHA RUHUWIKO

0

Mkuu wa mkoa wa Ruvumhindi waliopeleka mahindi yao katika kituo cha kuuzia mahindi Mgazini kata ya Kilagano wilaya ya Songea ambapo amepiga marufuku wafanyabiashara kuuza mahindi yao kwa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA badala yake ameagiza wakulima wadogo ndiyo watakaouza mahindi katika vituo vilivyotengwa,kulia Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema.

Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda katikati akizungumza na baadhi ya wakulima wa mahindi katika kijiji cha Mgazini kata ya Kilagano Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kuangalia kazi ya ununuzi wa zao hilo unaofanywa na wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA kanda ya Songea,kushoto Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge na kulia Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema

…………………………….

SERIKALI imesitisha kazi ya ununuzi wa mahindi katika kituo Kikuu cha Ruhuwiko katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, iliyokuwa inafanywa na wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula(NFRA) kanda ya Songea.

Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini na kujiridhisha kuwa, mahindi mengi yanayopelekwa katika kituo hicho ni ya
wafanyabiashara na sio wakulima ambao wamelengwa kunufaika na bei ya Sh. 500 kwa kilo moja.

Uamuzi huo umetolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibege,aliyeambatana na Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda wakati akikagua kazi ya ununuzi wa mahindi unaofanywa na wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa chakula(NFRA)kanda ya Songea katika wilaya ya Songea na Mbinga.

Badala yake amesema,kituo hicho kitumike kupokea mahindi ya wakulima yanayonunuliwa kutoka katika vituo vingine vya vijijini.

“serikali haiwachukii na wala haina ugomvi na wafanya biashara isipokuwa imefikia uamuzi huo ili kuwafikia,kuwalinda na kuwasaidia wakulima wasiokuwa na uwezo wa kupeleka mahindi nje ya nchi ili fedha watakazopata ziweze ziendelee kuongeza uzalishaji kwa msimu ujao”amesema.

Hata hivyo,ameruhusu mahindi yaliyopo katika kituo hicho ambayo yamekaa kwa muda mrefu na wamiliki wake wameorodheshwa na NFRA yanunuliwe na ambayo yameletwa baada ya apo yaondolewa katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amesema, katika msimu wa kilimo 2020/2021 mkoa huo umezalishaji tani milioni 1,623,510 ya mazao ya chakula, biashara na bustani kati ya lengo la kuzalisha tani 1.785,500 sawa na asilimia 91.

Amesema, kati ya hayo uzalishaji wa mazao ya chakula nit ani 1,384,705,mazao ya biashara tani 67,772 na mazao ya bustani zilizalishwa jumla ya tani 158,795.

Kwa mujibu wake, mkoa wa Ruvuma hadi sasa una chakula cha kutosha na kinachoendelea kutumika kilizalishwa katika msimu 2020/2021ambapo jumla ya tani 1,384,705 zilizalishwa.

Hata hivyo amesema, mahitaji ya chakula kwa wakazi wa mkoa huo ni tani 470,000 na kubakiwa na ziada ya tani 914,705 ambayo imeendelea kuuzwa kwa ajili ya kuwapatia wakulima kipato.

Aidha amesema, msimu 2020/2021 mahindi yamenunuliwa kupitia soko la huria na taasisi za Serikali ambazo ni wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa chakula(NFRA) na Bodi ya mazao mchanganyiko(CPB).

Amesema, katika awamu ya kwanza NFRA imenunua jumla ya tani 60,000 kati ya lengo la kununua tani 32,000 kwa wastani wa bei ya Sh.500 kwa kilo moja kwenye kituo kikuu na Sh.470 kwenye vituo vilivyoko vijijini na katika awamu ya pili NFRA kanda ya Songea imepewa lengo la kununua tani 35,000 kwa bei ya Sh.500 kwa kilo kwenye vituo vyote.

Kwa upande wake, Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda amemshukuru Rais Samiha Suluhu Hassan kwa kuongeza kiasi cha Sh. Bilioni 50 ili kununua mahindi ya wakulima ambapo kwa kanda ya Songea wameongezewa tani 35,000 kutoka tani 6,000 za awali.

Amesema, dhamira ya Rais Samiha ni kuona fedha hizo zinawafikia moja kwa moja wakulima na sio wafanyabiashara ambapo amempongeza Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kwa usimamizi mzuri wa ununuzi wa mahindi.

Amesema, bei ya Sh.500 kwa kilo ni ruzuku iliyotolewa na Serikali ili kila mkulima aweze kupata bei hiyo badala ya kuwanufaisha watu wachache wanaonunua mahindi ya wakulima kwa bei ndogo na kwenda kuuza kwa NFRA.

Profesa Mkenda amefafanua kuwa,utaratibu wa sasa kila mkulima atapata nafasi ya kuuza gunia 100 na sio vinginevyo na kueleza kuwa,wale watakaokosa nafasi hiyo wanaweza kuuza mahindi kwa Bodi ya mazao mchanganyiko(CPB)ambayo itaanza shughuli zake hivi karibuni.