Home Michezo MTIBWA SUGAR YAMTANGAZA OMOG KUWA KOCHA MPYA

MTIBWA SUGAR YAMTANGAZA OMOG KUWA KOCHA MPYA

0

KLABU ya Mtibwa Sugar imemtangaza Mcameroon Joseph Marius Omog kuwa kocha wake mpya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mcameroon huyo amewahi kuzifundisha kwa mafanikio klabu za Azam FC akiipa ubingwa wa Ligi Kuu na Simba SC akiwapa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).