Home Mchanganyiko SERIKALI KUOKOA BILIONI 33 MANUNUZI DAWA, VIFAA TIBA NJE YA NCHI.

SERIKALI KUOKOA BILIONI 33 MANUNUZI DAWA, VIFAA TIBA NJE YA NCHI.

0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Daniel Chogolo, akitoa Hotuba yake ya kuipongeza Wizara ya Afya kwa jitihada za kuboresha Sekta afya nchini kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM

 Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima,  akipata Maelezo mafupi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Meja Jeneral..

Waziri wa Afya Dkt Dorothy Gwajima,  akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya kukutembelea kiwanda cha Dawa Idofi kilichopo Njombe 

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima,  akitoa maelezo Mafupi kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Daniel Chongolo muda mfupi kabla yakumkaribisha kuongea na umma uliohudhuria Kwemye Ziara hugo.
*****************************
Na WAMJ.- NJOMBE
 Serikali inatarajia kuokoa zaidi ya bilioni 33 ambazo ilikuwa ikitumia kununua dawa na vifaa tiba nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Hayo yalielezwa na waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ukaguzi wa kiwanda cha kutengeneza mipira, dawa za vidonge na maji kilichopo kijiji Idofi mkoani Njombe.
Dkt. Gwajima amesema kiwanda hicho kinakwenda kuzalisha mipira ya mikononi (Gloves) ambayo kwa kipindi hiki imekuwa tatizo kubwa hasa kutokana naCovid 19.
Amesema mipira hiyo imekuwa shida na ghali na wakati mwingine kukosekana kabisa hivyo kiwanda hicho kinakwenda kutatua tatizo hilo la muda mrefu.
Ameongeza mipira itakayozalishwa kwenye kiwanda hicho ni zaidi ya mipira milioni mia moja na nne ambayo  inakidhi mahitaji ya Nchi.
“Mhe.Katibu Mkuu, uwezo wetu wa kuzalisha hapa nchini ulikuwa chini ya asilimia 20 lakini tunakwenda kupandisha uwezo wa uzalishaji kupitia kiwanda hiki” amesema Dkt Gwajima.
Dkt. Gwajima ameongeza kuwa serikali itatumia bilioni 8 .1 kupata huduma ya dawa na vifaa tiba kupitia kiwanda hicho tofauti na sasa ambapo inahitajika bilioni 34.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema ameridhishwa na ujenzi wa kiwanda hicho kwani unakwenda kutatua matatizo ya kukosekana kwa dawa na vifaa tiba hapa nchini.
Amesema yanayofanywa na MSD ni Mapinduzi ya kusaidia nchi kuepuka kutopoteza fedha za kigeni zilizokuwa zinatumika kuagiza dawa nje ya nchi.
“Utaratibu huu wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini utasaidia kuokoa zaidi ya bilioni 54.4 ambazo zilikuwa zitumike kununua vifaa hivyo nje ya nchi ndani kipindi cha mwaka mmoja” Amesema Chogolo na Kuongeza.
“Uamuzi wa kushusha kuagiza dawa hizi kutoka 50 mpaka 21 bilioni hayo ni Mapinduzi makubwa” alisisitiza Chongolo.
Naye Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga yeye ameiomba serikali kuharakisha ulipaji wa fidia kwa  wananchi wa kijiji cha Idofi ambao maeneo yao waliyatoa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Amesema wananchi hao wamelitoa zaidi ya shilingi milioni mia nane lakini wanadai kiasi cha fedha ambacho ni zaidi ya bilioni mbili.
“Tunaomba serikali yetu inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wananchi hawa ili waweze kulipwa fidia zao” alisema Sanga.