Home Mchanganyiko UJERUMANI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAKUMBUSHO YA TAIFA

UJERUMANI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAKUMBUSHO YA TAIFA

0

***********************************

Na Sixmund J. Begashe

Ujerumani kuendelea kushirikiana na Mkumbusho ya Taifa katika nyanja ya Utafiti, maonesho, kubadilishana uzoefu na program mbalimbali ili kuendeleza uhifadhi wa urithi wa kihistoria, Mambokale na utamaduni kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kikao hicho maalum Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kutoka nchini Ujerumani Bw Robert Doelger aliye ambatana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe Dkt Regina Hess kililenga katika kuyatazama mashirikiano ya sasa na kuona fursa zaidi za mashirikiano mengine.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbuaho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa wana matarajio makubwa kutokana na ujuio wa Mhe Doelger kwani katika mazungumzo yao wamegundua kuwa ipo mikusanyo mingi ya kihistoria iliyotoka Afrika hususani Tanzania ambayo imehifadhiwa nchini Ujerumani ambayo haikujulikana huko nyuma, hivyo itapanua wigo wa mashirikiano na taasisi zenye mikusanyo hiyo.

Naye Balozi wa Ujerumani Nchini Mhe Dkt Regina Hess ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa jitihada mbalimbali inazozichukuwa katika kuhifadhi urithi wa kistoria, wa Mambokale na wakiutamaduni ambao ni muhimu zaidi kwa kuelimisha jamii juu ya mahusiano kati ya Tanzania na Ujerumani.

Tumepata nafasi nzuri ya kuzungumza na uongozi wa Makumbusho ya Taifa juu ya Mambo muhimu yanayohusu mashirikiano katika uhifadhi wa urithi wa Historia, pia mgeni wetu Mhe Doelger amefurahi sana kuona maonesho mbalimbali ya chimbuko la Mwanadamu, Historia, Sanaa nk, tuliona tumlete hapa ili ajionee mwenyewe maana sisi tumesha fika hapa mara kadhaa” Alisema Balozi Steinbrenner.

Mkuu wa Idara ya Program Bwana Chance Ezekiel, amesema ujio wa wageni hao umezidi kufungua milango ya mashirikiano hasa katika mausala ya program mbalimbali hususani za Sanaa kwani hadi sasa yapo mahusiano mazuri kati ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani hapa nchini.