Home Mchanganyiko DC MOYO: WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOPATA MIMBA KUSAKWA POPOTE WALIPO

DC MOYO: WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOPATA MIMBA KUSAKWA POPOTE WALIPO

0

Mkuu wa wilaya
ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Luhota juu ya madhara ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wanaosoma katika shule zote za kata hiyo

Mkuu wa
wilaya
ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Luhota juu
ya madhara ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wanaosoma katika shule
zote za kata hiyo

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

Mkuu wa wilaya ya Iringa ameagiza
kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi wane waliopata ujauzito katika shule ya
sekondari Luhota wakijumuishwa na wazazi wa watoto wa kiume waliowapa ujauzito
ikiwa ni hatua ya kukomesha vitendo vya kuwaficha wanaotuhumiwa na vitendo
hivyo.

Hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya
Iringa imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na baadhi ya wazazi katika mikutano
ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vya Tagamenda na Kilambo baada ya wazazi
hao kudai kuwa wanafunzi wa kike wamekuwa wakiacha mimba kutokana na kupata
ujauzito wakiwa shuleni.

Wakizungumza kwenye mkutano wa
hadhara baadhi ya wazazi hao walisema kuwa wanafunzi wengi wa kikke katika kata
ya Luhota wamekuwa hawazifikii ndoto zao kutokana na kukatisha masomo mara
baada ya kupata ujauzito wakiwa mashuleni na hakuna hatua za kisheria ambazo
zimekuwa zikichukuliwa kwa watuhumiwa.

Wazazi hao walisema kuwa
wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule ya sekondari ya Luhota wamekuwa na
asilimia ndogo ya kumaliza masomo yao kutokana na wanafunzi hao kukumbana na
vishawishi vingi wanapoenda shule ni kusoma.

“Moja ya sababu zinazopelekea
changamoto hiyo ni umbali Mrefu wa naotembea watoto kufuata shule pamoja na
kutochukuliwa hatua kwa watu wanaohusika na mimba hizo hatua hiyo inayochechea
kulichukulia jambo hilo la kawaida na kuzoeleka kwa wananchi wa vijiji vya kata
ya Luhota” walisema wazazi

Aidha wazazi hao walimuomba
mkuu wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawachukulia hatua kali wanaume wote
ambao wamekuwa wanawapatia ujauzito wanafunzi hao kwa kuwa kufanya hivyo ni
kama kosa la jinai na watu hao wanatamkiwa kufungwa kwa mujibu wa sharia na
katiba ya nchi inavyotaka.

Akielezea kuhusiana na matukio
ya wanafunzi hao kupata ujauzito wakiwa shuleni, Mkuu wa Shule ya Sekondari
Luhota iliyopo katika Halmashauri ya Iringa Lesiyo Kisonga kuwa jumla ya
wananfunzi wanne wamepata ujauzito katika kipindi cha mwezi wa kwanaza hadi
mwezi wa tisa jambo lililowapelekea kufukuzwa shule kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kuwa changamoto ya wanafunzi
wengi imekuwa inajitokeza mara kwa mara kutokana na wazazi kushindwa kutoa
ushahidi katika mamlaka husika baada ya watoto wao kugundulika kuwa wamepata
ujauzito wakiwa shuleni jambo ambapo limepelekea wanaume wengine kuwa jambo
hilo ni la kawaida kwao.

“Moja ya changamoto
zinakwamisha mapambano ya kuzuia mimba shuleni ni kukosekana kwa ushahidi na
ushirikiano kutoka kwa wazazi na watoto wenyewe kukataa kumtaja mhusika wa
ujauzito ambao amekuwa amepewa na wanaume huyo” alisema Kisonga

Kwa upande wake mkuu wa wilaya
ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliliajiza jeshi la polisi wilaya ya Iringa
kuhakikisha wanawakamata wazazi wote wa wototo wanne waliwapatia ujauzito na
watoto wenye ujauzito kwa lengo la kukomesha matukio hao.

Alisema kumekuwa na wazazi
ambao wamekuwa wanafanya makubaliano kifamia huku wakiwa wanakatiza ndoto za
wananfunzi hao wa kike hivyo lengo la kuwakamata wazazi hao wote ili kupunguza na
kumaliza tatizo la kuwapatia ujauzito wanafunzi hao.

Moyo alisema kuwa lengo la
kuwakamata wote hao ni kuhakikisha ushaidi haupotei wala keshi hizo haziishii
ngazi za familia kama ambavyo inafanyika hivi sasa kwenye jamii nyingi za
wananchi wa wilaya ya Iringa na kusema kuwa Iringa bila mimba za utoto
inawezekana.

Aliwataka viongoziwa
vijiji,mtaa,kata na tarafa kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi
la polisi ili kukamilisha ushaidi wa keshi hizo na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria kwa lengo la kumaliza tatizo la mimba za utotoni.

Jumla ya Mimba nne zinatajwa
kutokea katika kipindi cha mwezi January hadi September mwaka huu jambo
linalorudisha nyuma ndoto za watoto wa kike.