Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Ilala Bw.Ubaya Chuma akizungumza katika Mahafali ya Nane ya Chuo cha Furahika Education College yaliofanyika jana Ilala Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Ilala Bw.Ubaya Chuma akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo cha Furahika Education College katika Mahafali ya Nane ya Chuo hicho yaliofanyika jana Ilala Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Furahika Education College Bw.Sound Kassim akizungumza katika Mahafali ya Nane ya Chuo cha Furahika Education College yaliofanyika jana Ilala Jijini Dar es Salaam
Madiwani wa Viti maalumu mkoa wa Ilala wakiwa katika Mahafali ya Nane ya Chuo cha Furahika Education College yaliofanyika jana Ilala Jijini Dar es Salaam
Wahitimu wa Chuo cha Furahika Education College wakiwa katika Mahafali ya Nane ya Chuo hicho yaliofanyika jana Ilala Jijini Dar es Salaam
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo.
Wanafunzi wa Chuo cha Furahika Education College wakitoa burudani kwa wahitimu wa Chuo hicho.
*******************************
MWENYEKITI Wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ilala Bw.Ubaya Chuma amesema kuwa katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu itakayomsaidia katika kujikimboa kiuchumi kwa kushirikiana na madiwani wa jimbo hilo watashirikiana na chuo cha Maendeleo ya Viwanda, Ujuzi na Ubunifu cha Furahika Education College kwa kuwahimiza wazazi na mabinti kujifunza kozi mbalimbali zinazotolewa bure na chuo hicho.
Akizungumza katika mahafali ya nane ya chuo hicho Ubaya amesema, atashirikiana kwa ukaribu na madiwani wa jimbo na Wilaya zote za Mkoa huo katika kuhakikisha chuo kinapata wanafunzi wa kutosha pamoja na walimu ili kuweza kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi.
“Kupitia madiwani naamini jambo hili tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa, nawaomba wawakilishi wa madiwani mliopo hapa, mkayafikishe haya kwa jamii, elimu inatotolewa bure kwa mabinti zetu na uhakika wa kupata ajira upo.” Amesema.
Aidha amesema, wazazi na walezi wawasaidie walimu katika suala la maadili kuanzia nyumbani ili kujenga vijana imara kwa taifa na jamii kwa ujumla.
“Nimekubali kuwa mlezi wa chuo cha Furahika, wazazi na walezi tushirikiane katika hili ili na kuepusha changamoto tunazoweza kuzikabili ikiwemo mimba za utotoni na nyendo zisizofaa.” Ameeleza Ubaya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Bw.Sound Kassim amesema chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali bure kwa watoto wa kike ikiwemo ufundi, mafunzo ya hoteli, kompyuta, muziki naa lugha za kigeni ikiwemo kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kichina na kuwataka madiwani kupeleka fursa hizo katika kata zao ili mabinti hao waweze kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia kujikimboa kiuchumi
Aidha amesema kuwa malipo yanayochangiwa na wanafunzi hao ni ada ya mtihani wa taifa pekee, huku masula ya chakula na malazi kwa baadhi ya wanafunzi yakisimamiwa na chuo hicho kupitia ufadhili.