Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Mohammed Gwae, akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii baada ya kutambulishwa kwa Wajumbe kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati hiyo. Kikao hicho kilifanyika leo Septemba 10, 2021, jijini Dodoma.
Mwenyekiti huyo aliwaambia Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni wajibu wao kufuata sheria na kumshauri Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Aloyce Musika, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Idara ya Huduma za Uangalizi katika Kikao cha Kamati hiyo, kilichoifanyika, jijini Dodoma, leo.
Katibu huyo alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi kufikia Julai 2021, Idara imefanikiwa kuwasajili Wafungwa 3496 na kuwawezesha kutumikia adhabu nje ya magereza hivyo kupunguza msongamano magerezani.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii wakiwa katika Kikao cha Kamati hiyo, kilichofanyika leo Septemba 10, 2021, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Mohammed Gwae (wapili kulia), Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Aloyce Musika (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma leo.