Mjumbe wa Bodi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangila,akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili.
Meneja usimamizi miradi ya REA, Mhandisi Romanus Lwena,akitoa maelekezo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Muonekano wa nguzo ya umeme.
Mjumbe wa Bodi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Styden Rwebangila,akitoa majumuisho kwa waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Meneja usimamizi miradi ya REA, Mhandisi Romanus Lwena,akielezea Mradi ulipofikia wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma, Donasian Shamba,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Mkandarasi wa Mradi Mhandisi Sangora Mollel,akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Kongwa
Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Mhandisi Styden Rwebangila,amekiagiza kitengo cha uhamasishaji kuweka jitihada katika kutoa hamasa kwa wananchi ili waweze kuchangamkia fursa kuunganishiwa umeme vijijini.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Mhandisi Rwebangila,amesema kuwa licha ya serikali kuwekeza fedha nyingi katika miundombinu ya umeme katika maeneo ya vijijini bado mwitiko ni mdogo wa wananchi kuunganisha huduma ya umeme katika nyumba zao.
“Changamot tumeiona na sisi kama Bodi tunakiangiza kitengo cha uhamasishaji kuja huku kwa wananchi ili kutoa hamasa kwa wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa umeme.”amesema Mhandisi Rwebangila
Mhandisi Rwebangila amesema kuwa kutokana na ziara hiyo wamebaini bado wananchi wengi hawajanufaikiwa na huduma hiyo licha ya miundombinu ya umeme kupita jirani na makazi yao.
“Bodi pia tumeridhishwa na kasi ya mkandarasi kwani hadi sasa amifikia asilimia 64, ya mradi na kuvuka lengo ambalo lilikuwa ni asilimia 48, hadi kufikia sasa”aamesema
Aidha amesema kuwa katika miradi ya ujazilizi awamu ya pili A, zaidi ya vitongoji 349, vya mkoa wa Dodoma vitanufaika kwa kufikishiwa huduma hiyo ya nishati ya umeme.
Kwa upande wake Meneja usimamizi miradi ya REA, Mhandisi Romanus Lwena,amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuunganisha umeme kwa gharama ya sh.27,000 ili kuanzisha miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato.
Naye Kaimu meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma, Donasian Shamba,amesema kuwa wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Bodi huku akiahidi kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha wananchi wote waliofikiwa na miundombinu wanapata umeme.
Awali Mkandarasi wa mradi Mhandisi Sangora Mollel,amesema kuwa watakamilisha mradi huo kwa wakati mwezi Aprili mwakani.
”Kwa sasa mimi kama Mkandarasi sina hivi changamoto kubwa ambayo inaweza kuwakwamisha kukamilisha mradi huo kwa wakati”amesema Mhandisi Mollel