Home Mchanganyiko MKUU WA WILAYA MSTAAFU ATAKIWA KULIPA FIDIA YA MILIONI 100 KWA TUHUMA...

MKUU WA WILAYA MSTAAFU ATAKIWA KULIPA FIDIA YA MILIONI 100 KWA TUHUMA ZA KUDHALILISHA

0

*****************************

Na Lucas Raphael,Tabora

ALIYEKUWA mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick Kitwala amepandihwa kizimbani katika mahakama ya wilaya akikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha mtumishi wa mamlaka ya maji safi na maji taka Tabora (TUWASA) Alex Ntonge na kutakiwa kulipa fidia ya sh milioni 100.

Akisoma hati ya mashitaka hayo katika mahakama hayo majira ya saa 03:30 asubuhi ya kesi ya madai namba 04/2021 chini ya hakimu Nzige Sigwa wakili wa mlalamikaji Kevin Kayaga aliambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa ama mshitakiwa alitenda kosa hilo la udhalilisha nyumbani kwa mlamikaji.

Wakili Kayaga aliendelea kudai kuwa mnamo mwezi januari 5,mwaka huu mtuhumiwa akiwa na askari polisi wenye silaha za moto alifika nyumbani kwa Alex Ntonge ambaye ni mlalamikaji na kufanya matukio kadhaa ambayo mlalamikiaji amedai ni udhalilishaji mbele ya familia yake na Jamii kwa ujumla.

Aidha,upande huo wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa baada ya matukio hayo ambayo mlalamikaji amedai kutotetendewa haki na kudhalilishwa alikamatwa na askari na kupelekwa selo kwa kosa ambalo hadi sasa hajui alitenda kosa gani.

Aidha,kufuatia matukio hayo mlalamikaji amefungua madai haya akiomba mtuhumiwa kumlipa fidia ya sh milioni 100 kwa kile ambacho anaona hakustahili kufanyia hayo hata kama angewa na kosa kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wa wakili wa mtetezi wa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Tabora Kitwala Erick Komanya,Saikoni Justine alisema mteja wake anaiomba mahakama hiyo kuwa apewe muda ili aandaye maelezo yake kimaandishi na atayawasilisha mahakamani hapo mwezi septemba 6 mwaka huu ombi ambalo mahakama hiyo iliridhia.

Aidha,akiaarisha shauri hilo hakimu wa mahakama wa wilaya Nzige Sigwa alisema kufuatia ombi la mshitakiwa anakubali kutoa muda huo wa siku alizoomba na kesi hiyo itatajwa mwezi septemba 23 mwaka huu.

Hata hivyo kabla ya shauri hilo kuanza kusikilizwa mlalamikaji alikuwa akimpiga picha aliyekuwa mkuu wa wilaya hali ambayo ilitaka kuleta tafrani huku mtuhumiwa akitoa vitisho kadhaa, lakini ilikuwa shwari baada ya busara kutumika.